Airtel yazindua ofa kabambe kupiga simu kwenda nje ya nchi
• Wateja kupata kifurushi cha dakika 25 kupiga simu kwenda India
• Ofa hii inapatikana masaa 24 siku 7 za wiki,
Kampuni ya Bharti (“Airtel”) inayoongeza kwa kutoa huduma za mawasiliano inayoendesha shughuli zake katika nchi 20 barani Afrika na Asia leo imetangaza uzinduzi wa ofa itakayo wawezesha wateja wa Airtel Tanzania kupiga simu kwenda nje kwa gharam nafuu zaidi.
Ofa hii inaendelea kuonyesha dhamira ya Airtel Tanzania ya kuendelea kuwanganisha watanzania katika mtandao wa mawasiliano na kuwapa huduma bora zenye gharama nafuu. Uzinduzi huu unafatia utambulsho wa huduma kabambe ya Airtel yatosha iliyofanyika week chache zilizopita.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya, Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwn. Sunil Colaso alisema ”baada ya uzinduzi wa mafanikio ya huduma yetu ya Airtel yatosha. leo tunazindua ofa ya mawasiliano ya gharama nafuu na kuwawezesha wateja wetu kuwasiliana na familia ,marafiki na washirika wa kibiashara walioko nje ya mipaka ya nchi.
Kwa kiasi cha chini cha hadi shilingi3, 000 sasa wateja wa Airtel wanaweza kupiga simu India masaa 24 kwa siku 7 za wiki. Ofa hii itampatia mteja dakika 25 za muda wamaongezi kwa muda wa wiki nzima.
Aliongeza “Hii ni ya kwanza kutoka Airtel, na tunaendelea kuwahakikishia wateja wetu nchi nzima huduma bora, za uhakika na gharama nafuu za mawasiliano wakati wote. Tumesikiliza kile wateja wetu wanachokitaka na kutengeneza ofa inayokidhi mahitaji yao hivyo tutaendelea kutekeleza dhamira kwa watanzania ya kuleta huduma zenye ubunifu, bora na gharama nafuu ambazo kwa uhakika zitaleta uhuru wa kuongea nje ya mipaka.
Ofa hii itawawezesha wateja wanaosafiri au kuwasiliana na India iwe kimasomo, kibiashara , wanaotembelea India kimatibabu kuwa na mawasiliano na familia zao kwa gharama za kiushindani zilizo nafuu zaidi. Uzinduzi huu ni mwanzo wa kuleta mapinduzi ya mawasiliano katika soko la Tanzania.
Kwa upande wake Balozi wa India nchini Tanzania, H.E. Mr.Debnath Shaw alisema” Tunawapongeza Airtel kwa kuzindua ofa hii itakayoendelea kutuunganisha na kuendeleza ushirikiano wetu kati ya India na Tanzania. nchi hizi mbili zimekuwa na ushirikiano wa karibu si kibiashara tu bali katika sekta ya elimu, Afya na shughuli nyingine za kijamii.
Ninayofuraha kuona Airtel ikiwa mstari wa mbele kuleta gharama nafuu katika soko la Tanzania. Nchini India Airtel ni mtandao unaoongoza uliowekeza katika technologia ya hali ya juu, mtandao bora na unaotoa huduma bora za gharama nafuu kwa wateja wake. Ninayofuraha kuona huduma za mawasiliano zinabadilika kwa kasi na kufanana kama za India katika soko la Airtel barani Afrika.”
“Tunaamini hii ni fulsa pekee kwa wafanyabiashara , wanafunzi waliko India na wengine wanaotembelea India kwa sababu mbalimbali kuwasiliana na familia, marafiki na washirika wa kibishara waliko Tanzania kwa
gharama nafuu
Akifafanua kuhusu ofa hii Meneja wa biashara za kimataifa wa Airtel bi Prisca Tembo alisema” ofa hii inapatikana katika kifurushi cha muda wa maongezi ambapo kwa bei moja ya shilingi 3000 mteja atapata dakika 25 atakazozitumia masaa 24 kwa siku 7. Kifurushi hiki kitatozwa kwa sekunde na kudumu kwa muda wa wiki nzima. Sambamba na hilo, Simu zitakazopigwa kwenda nchi nyingine nje ya ofa hii zitatozwa kwa bei ya kawaida”
“Ili kujiunga na ofa hii mteja anatakiwa kupiga*149*13# na kuweza kufurahia ofa hii. Na huduma hii ni kwa wateja wa malipo ya awali nchi nzima” aliongeza Tembo
Hivi karibuni Airtel ilizindua huduma ya Airtel yatosha inayotoa ofa ya vifurushi vya muda wa mongezi, ujumbe mfupi na internet zinavyomuwezesha mteja kuwasiliana na mtandao wowote nchini. Ikiwa katika mwendelezo wake wa kuboresha huduma zake Airtel imezindua ofa mpya ya kupiga simu kwenda nje ya nchi inayompatia mteja kifurushi cha muda wa maongezi kupiga simu kwenda India. Ili kupata huduma hii piga *149*13# na unganishwe sasa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.