Wanamabadiliko.
Ndugu zangu kutokana
na hali ya nchi yetu kukumbwa na changamoto mfululizo na lawama zote tunambebesha
Rais kusema ni nchi yake peke yake tunakosea, tujitahidi kumpa mawazo nini
kifanyike wapi parekebishwe ili kujenga nchi. Tukikaa kimya eti tunasubiri sijui
chama tawala king`atuliwe madarakani hivi navyo tunakosea.
Nchi ni yetu na sio ya
mtu mmoja, Rais tulimchagua wenyewe kwa
mapenzi yetu, cha msingi katika hiki kipindi chake kilichobaki madarakani
anahitaji msaada wa mawazo na sio lawama kama tunavyokesha kukilaumu chama
tawala na uongozi wake.Kulaumu sio solution, solution ni kusaidiana wapi
kakwama apate msaada na pindi tunapo fanikisha tumefanikiwa sote.
Lawama zisizokwisha
kila kukicha hazisaidii ndugu zangu,Kikwete sio malaika wa kusema kila kitu
anaweza na yeye ni binaadamu hajakamilika.
Nina imani kubwa hata
hatakayekuja hataweza kuwaridhisha wanzatania wote mnavyotaka,cha msingi tuwe
na tabia ya kutoa maoni nini kifanyike kwa viongozi wetu ili kujenga nchi na
sio lawama ndugu zangu.
Nina Imani kubwa sana
na watu wa jukwaa hili kwamba wana fikra nzuri za kumshauri kiongozi
yoyote yule ili kuleta maendeleo.Hata sisi kwenye jukwaa letu huwa tuna
taratibu zetu tukiona kwamba fulani anakosea huwa tunajaribu kumrejesha kwenye
njia iliyo sahihi na sio kumtupia lawama Moderator.
Nawaomba ndugu zangu
kwa heshima zote na upendo wangu kwenu tujaribu kumsaidia huyu kiongozi wetu
maana hata na yeye sidhani kama ana furaha na amani ndani ya nafsi yake kwa
lawama za kila mtu.
Tujenge misingi ya
kusaidiana kimawazo..najua wengi mmechoshwa na CCM na baadhi ya viongozi wao, sasa
basi tujipange tusije kupoteza hata hiki tulichonacho wakati tukisubiri chama
hicho kingine ambacho kitashika hatamu 2015, ila ninatoa angalizo, tusije
tukaacha kuwasaidia hata hao watakaokuja kutuongoza kwa fikra kuwa wao tu ndiyo
kila kitu.
Yangu ni hayo tu, nawatakia
kila la heri.
Maganga One.
Tupe maoni yako
UJUMBE HUU UNGEMTUMIA NA NDUGU YETU AMBAYE TANGU NIMTAMBUE SIJAMSIKIA AKISIFIA CCM INGAWA KUNA MENGI TU CCM IMEYAFANYA NA SI MWINGINE NI SLAA
ReplyDelete