HUKU AKIVIFANANISHA VYOMBO VYA HABARI NA DARAJA MGENI RASMI KTK UFUNGUZI WA SEMINA HIYO YA MFUKO WA PENSHENI WA PPF ILIYOFANYIKA LAKAIRO HOTEL MWANZA, AMEISHUKURU PPF KUTAMBUA UMUHIMU WA VYOMBO VYA HABARI KTK KURAHISISHA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA SERIKALI KWA JAMII.
PICHANI WADAU WA PPF MWANZA.
USHINDWE MWENYEWE KWANIIII... MFUKO WA PPF UMEBORESHA HUDUMA ZAKE KWA WANACHAMA PAMOJA NA KUONGEZA MAFAO YAKE KUFIKIA SABA.
WAANDISHI WA HABARI KTK SEMINA.
KATIKA KIPINDI CHA MIEZI 6 OFISI YA KANDA IMETOA SEMINA ZA ELIMU KWA WANACHAMA WAKE WENGI KTK MIKOA YA KAGERA, SHINYANGA, TABORA, KIGOMA NA MARA VILEVILE IKITEMBELEA MAKAMPUNI YA UMMA NA BINAFSI AMBAPO PPF IMEGUNDUA KUWA BAADHI YAO HAWANA UFAHAMU JUU YA TARATIBU ZA MFUKO WA PENSHENI, SAMBAMBA NA TARATIBU ZAKE KWA UNDANI ZA UFUATILIAJI MAFAO AMBAZO SASA ZIMERAHISISHWA KWA MTEJA KUPATA HARAKA MAFAO YAKE PINDI ANAPO ACHA KAZI AU KUSTAAFU.
JIMMY LUHENDE, MWENYEKITI MPC.
"SERIKALI ITAMBUWE KUWA WAANDISHI WA HABARI ILI WAFANYE KAZI YAO VIZURI NA KWA UHAKIKA WANAHITAJI PROTECTION" (HILO NALO NENO!) PIA AMEISHUKURU PPF KWA KUTAMBUA THAMANI YA WAANDISHI KILICHOBAKI UTAKELEZAJI.
MWANA HABARI ROBERT.
KATIKA UTAMBULISHO JAMAA ALIWACHANA MBAVU WANASEMINA ALIJITAMBULISHA VYEO VYAKE VYOTE DUNIANI HADI NYUMBANI ANAPOISHI NA MWISHO AKAISHUKURU PPF KUTOA ELIMU KWA UMMA HASA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI JUU YA UMUHIMU WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII HUSUSANI KWA KUJIUNGA NA MFUKO WA PPF.
MESHARK BANDAWE ZONAL MANAGER.
MBALI NA KUWAASA WANDISHI WA HABARI KUWAFICHUA WAAJIRI WANAOKWEPA KUJIUNGA NA MFUKO WA HIFADHI AMBAPO WAFANYAKAZI HUKOSA HAKI ZAO Z MSINGI KWA MUJIBU WA SHERIA ALIONGEZA:- "MFUKO WA PENSENI ULIANZISHWA MWAKA 1978. AWALI UKILENGA ZAIDI WAFANYAKAZI WALIOAJIRIWA KTK MASHIRIKA YA UMMA LAKINI KWA SASA MFUKO UNARUHUSU WAAJIRI NA WAJIRIWA KUTOKA MAKAMPUNI BINAFSI PAMOJA NA WALE WALIOJIAJIRI WENYEWE KTK SEKTA ZISIZO RASMI KUJIUNGA NA MFUKO HUU"
LENGO AU MADHUMUNI YA MFUKO HUU NI KUTOA KINGA YA HIFADHI YA JAMII HUSUSANI MAFAO YA PENSHENI BAADA YA MTUMISHI KUTIMIZA UMRI WA KUSTAAFU KAZI. SAMBAMBA NA KUSIMAMA KAMA KINGA KWA MAJANGA MBALIMBALI.
MAELEZO ZAIDI TEMBELEA www.ppftz.org
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.