ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 11, 2010

POWER BREAKFAST YAVUMBUA JIWE LINALOCHEZA (NYABUREBHEKA ) UKARA WILAYANI UKEREWE.

MTARI, KIJANA ALIYE RISISHWA NGUVU YA JIWE HILO LA UKOO.

MJI WA MWANZA.

NILITOKA MWANZA SIKU YA J3 SAA 3:00 NA MV CLARIUS NI MWENDO WA MASAA MA3 HADI KISIWA CHA NANSIO UKEREWE KISHA NIKAELEKEA BUGORORA ENEO LA KIVUKO KINGINE MWENDO WA DK 20 TOKA NANSIO.
SAFARI KUELEKEA UKARA NA MV NYERERE.

ENEO HILI LA BUGORORA NDIPO KINAPOPATIKANA KIVUKO CHA KUELEKEA KISIWA CHA UKARA MWENDO WA SAA 1.

MJI WA BWISHA UKARA.

TOKA BWISHA UKARA SAFARI KWA PIKIPIKI HADI KIJIJI CHA NYANG'OMBE AMBAKO NIKAKUTANA NA KIJIJI CHA MZEE MAKOROKORO. MZEE AMBAYE UMRI WAKE UMEKWENDA MIGUU IMECHOKA AKITEMBEA KWA KUJIVUTA. ANA KIJANA WAKE AITWAE MTARI AMBAYE ALIPOTIMIZA MIAKA 10 ALIRISISHWA KIMILA NGUVU ZA JIWE LA 'BUREBHEKA'.KIJANA SASA ANA UMRI WA MIAKA 20.

WATU WA MTAA WA DUKE WAKICHEZA KARATA SEBULE KUU.

KIJANA MTARI NDIYE ALIYEKUWA MGENI WETU MIE NA DREVA WANGU WA PIKIPIKI, NAE AKATUTOA PALE NYUMBANI HADI ENEO LA JIWE KWA PIKIPIKI MKAO WA MSHIKAKI (MWENDO WA NUSU SAA).
MTAA WA DUKE.

TUKAFIKA ENEO LA JIWE LINALOCHEZA NYAMANGA MTAA WA DUKE MTU AMBAYE ALIKUWA MAARUFU HATA WAKAPACHIKA ENEO HILO JINA LAKE (KAMA DAR ES SALAAM VILE MWANANYAMALA KWA HADIJA KOPA).
HAPA NA PALE MTAA WA DUKE.

MTAA WA DUKE SI MTAA KAMA UNAVYOWEZA KUDHANI KIMJINIMJINI ETI BARABARA, LA-HASHAA! NI ENEO LA UFUKWENI KWA WAVUVI.
JIWE LA BUREBHEKA LIKO KILIMANI HIVI JUU YA MIAMBA MIKUBWA MASHARTI KABLA YA KULIFIKIA JIWE KTK MLANGO WAKE WA NJIA UNAVUA VIATU UNAVIACHA HAPO, UNAPANDA HADI KWENYE JIWE.
NJIA KULIFIKIA JIWE.

MTARI AKIWEKA MCHANGA JUU YA FEDHA.

MARA KABAAAAN! JIWE HILI HAPA...TUKAWEKA SH 1000/= KISHA JUU YAKE UKAWEKWA MCHANGA. SHUGHULI IKAANZA KIJANA MTARI (HUKU AKILISUKUMA HIVI KULIZINDUA) AKALIZUNGUMZISHA AKILISIHI KWA LUGHA YA KUKARA KUCHEZA KWANI LIMEPATA WAGENI. DAKIKA KAMA SI SEKUNDE LIKAANZA KUNESA NA LIKAENDELEA ZAIDI NA ZAIDI. SIYO KWAMBA LINA NESA KIUBAVU HAPANA LINA NESA HASWAAA, KUTOKA PEMBE YA FEDHA INAPOWEKWA HADI KULE MBELE KAMA LINAJISUKUMA KUELEKEA ZIWANI. LIKAENDELEA KWA DAKIKA KADHAA KISHA LIKATULIA.

HUKU NIKIBISHA KIMOYOMOYO NAMI NIKAOMBA RUKSA KUJARIBU KULISUKUMA NIKIDHANI KUWA 'SI LINACHEZA KWASABABU KIJANA ANALISUKUMA. ...SUKUMA...SUKUMA... AAAAAH WAPI!! 'NGOMA IMEDINDA' JIWE HALICHEZI NG'O!

UNYAYO WA KAKA YAKE NA NYABUREBHEKA.

SIRI KUBWA YA JIWE LA NYABUREBHEKA KUCHEZA KWA MUJIBU WA MZEE MAKOROKORO ANASEMA KUWA MIAKA YA 1800 (historia haijahifadhiwa vyema) MTU NA KAKA YAKE WALIKUWA KATIKA SAFARI YA KUHAMA KUTOKA KOME UKARA KUELEKEA NYAMANGA MAKAO YAO YA ZAMANI, AMBAPO WALIACHA KUKU NA MBUZI NA MIFUGO MINGINE.(yale maisha ya kuhama hama),SASA KTK SAFARI YA KURUDI MAKAZI YA ZAMANI, MDOGO MTU AKAKANYAGA SEHEMU KWA MGUU WA KUSHOTO AKAPOTEA, KAKAYE AKAFIKA ENEO HILO AKAKANYAGA KWA MGUU WA KULIA HAKUDHURIKA.

KAKA MTU AKAMTAFUTA SANA MDOGO WAKE, KATU ASIPATIKANE. AKAAMUA KUREJEA NYUMBANI KUTOA TAARIFA NAO WAKAFIKA ENEO LA TUKIO, SAKA SANA WASIMPATE KIJANA WAO. HATA SIKU YA 2,YA 3 HADI WIKI, KIJANA KATU ASIONEKANE!

UNYAYO WA NYABUREBHEKA KIJANA ALIYEGEUKA JIWE.

KARAI LA KUNYWESHEA MIFUGO.

NDIPO WAKARUDI NYUMBANI KUFANYA TAMBIKO, TAMBIKO LIKAJIBU KUWA KIJANA WAO KAGEUKA JIWE PINDI TU ALIPO KANYAGA ENEO HILO KWA MGUU WA KUSHOTO.
MGANGA AKASEMA HAKUNA JINSI YA KUMREJESHA KIJANA ZAIDI YA WAO (WANANDUGU) KUMTEMBELEA (JIWE BUREBHEKA) KUFANYA TAMBIKO KILA BAADA YA MIAKA 4 KWA KUCHINJA MBUZI MWEUSI WANAYE MKUZA WAO MBUZI ANAYEKWENDA MALISHONI MWENYEWE WAO WAKIMPA HIFADHI YA KULALA TU.

MIE NA NYABUREBEKA.

INASEMEKANA KIPINDI CHA MIAKA YA NYUMA WAZUNGU WALIFIKA ENEO HILI NA MELI ZAO ZENYE NGUVU WAPATE KUTAFITI KISAYANSI NGUVU HIZO ZA JADI, WAKALIFUNGA MINYORORO NA KULIVUTA KWA MINAJILI YA KULITUPA ZIWANI, WAKACHEMSHA BAADA YA MINYORORO YAO IMARA KUKATIKA.

Tupe maoni yako

8 comments:

  1. G. Sengo post video clip bana

    ReplyDelete
  2. sasa mkuu tutaamini vipi kama linacheza siungechukua hata video yake unakula mzigo ukiwa live

    ReplyDelete
  3. stori nzuri sana kaka, hao ndio wakerewe

    ReplyDelete
  4. Nimeipenda sasa naona umefika wakati hilo eneo litangazwe kwaajili ya kuvutia watalii. safiiiiiiii!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. sa mbona hatulioni likicheza jamani si ungetuwekea video clip jamaa

    ReplyDelete
  6. Ni kweli kabisa G Sengo, tuwekee video clip tuhakikishe. Ikibidi fanya mipango urudi tena Ukara ili uturidhishe wadau.

    ReplyDelete
  7. Bila Video nitaendelea kusema 'siamini.'

    ReplyDelete
  8. ha ha haaa wala hukukosea hiyo ni nguvu za giza tu kama wasemavyo wakerewe ni hatari sana. hapo panatakiwa mzee wa upako ateremke hapo halafu watashuhudia wenyewe ha haa wakerewe bwana.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.