Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Prof. Honest Ngowi (aliyesimama) akizungumza katika Kongamano la Mwaka
la Uwezeshaji. Wengine picha ni watoa mada mbalimbali walioshiriki katika Kongamano hilo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akichangia nafasi ya Benki yake katika kuchagiza uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mnyororo mzima wa ongezeko la thamani katika kilimo
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN), Dkt. Jim Yonazi akizungumzia nafasi ya TSN katika kuwezesha juhudi za Serikali katika kuwawezesha wananchi kiuchumi ambapo alisema kuwa Shirika lake lina uwezo na teknolojia ya hali ya juu katika kuwafikia sehemu kubwa ya watanzania. Alitoa wito kwa taasisi za umma na binafsi kutumia nafasi hiyo kuwafikia walengwa wa huduma zao.
Baadhi ya Manaibu Mawaziri wakifuatilia mada wakati wa Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji.
Baadhi ya wadau wa taasisi za uwezeshaji wananchi kiuchumi wakifuatilia kwa makini Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji.

Na Mwandishi wetu, Dodoma
Wito umetolewa kwa Watanzania hasa kwa wadau
wanaojihusisha na uwezeshaji wananchi kiuchumi kubadili
mitazamo juu ya namna sahihi ya kuwawezesha wananchi hao katika
kutimiza lengo la serikali la kuwainua wananchi kiuchumi ili kuimarisha
kipato na kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.
Wakizungumza katika Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji
linalofanyika mkoani Dodoma wadau hao wamesema
kuwa kuna ulazima wa wadau hao kujua mahitaji sahihi ya wananchi
wanaohitaji huduma za uwezeshaji wa kiuchumi kwa kuwa kila kundi lina
mahitaji yake.
Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Prof. Honest Ngowi amesema
kuwa ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote unazingatia
mahitaji maalumu ya kila sekta ya kiuchumi na kutolea mfano kuwa
wakulima nchini hawahitaji rasilimali fedha pekee ili kuongeza tija
katika kilimo chao bali wanahitaji masoko ya uhakika ya mazao yao.
“Uzoefu kutoka kwa watekelezaji wa uwezeshaji wa wananchi
kiuchumi unaonesha kuwa rasilimali fedha
si kila kitu pekee katika kuwawezesha wananchi kiuchumi bali kila kundi
linahitaji mahitaji yake, mfano mkulima anahitaji soko la mazao yake
ili aweze kuongeza tija kwenye kilimo chake,” alisema Prof. Ngowi.
Akichangia mjadala
huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TADB),
Bw. Francis Assenga alisema kuwa Benki yake ina Dira ya kuwa benki ya
mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kwa
kuwawezesha wananchi kwa kuzingatia mahitaji maalumu kuendana changamoto
za kimaeneo hili kuwezesha wananchi kiuchumi nchini
ili kutekeleza kwa vitendo dhamira ya Serikali kuwafikisha wananchi
wake kufikia hadhi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
“Muundo wa TADB ni tija katika kuchagiza uwezeshaji wananchi kiuchumi hasa wakulima wadogo nchini
kwani Benki inafanyia kazi mnyororo mzima wa ongezeko la thamani katika kilimo kwa kutatua
changamoto mbali mbali kama vile kiwango kidogo cha uzalishaji; ukosefu wa mbinu na teknologia za
kisasa; matumizi madogo ya umwagiliaji,” alisema
Aliongeza:
“Changamoto nyingine ni ukosefu wa mtaji na upatikanaji wa mikopo kwa
wakulima; ukosefu wa masoko ya mazao; ufinyu wa bei za
mazao; miundo mbinu mibovu ya usafirishaji; maghala ya kuhifadhi mazao;
nishati ya umeme na miundombinu hafifu vijijini; ufinyu au kutokuwepo
kwa ongezeko la thamani kwa mazao ya kilimo; mabadiliko ya hali ya hewa;
na mmomonyoko wa udongo, pamoja na changamoto
zinginezo,” aliongeza.
Kuanza
kufanya kazi kwa Benki ya Kilimo kunaleta suluhisho la changamoto
nyingi zilizokuwa zinaikabili sekta kilimo na uwezeshaji wa wananchi
kiuchumi kama inavyowekwa bayana na dhima ya Baraza la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi ambayo inalenga kuwaongoza watanzania katika kujenga
uchumi wenye nguvu kwa kuboresha mazingira ya kibiashara na kutoa fursa
sawa za kiuchumi.
Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji linafanyika katika kutekeleza
Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
iliyoundwa mwaka 2004 na Sheria ya Uwezeshaji namba.16 iliyopitishwa na
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.