Ikiwa ni Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Act-Wazalendo Anna
Mghwira kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkao wa Kilimanjaro leo ameibuka Katibu
wa chama hicho Mkoa wa Mbeya Bahati Longopa na kutangaza kujiuzuluzu
nafasi hiyo kwa alichodai kutoridhia uteuzi huo.
Longopa amesema kuendelea kuwa kiongozi wa chama kutampa wakati mgumu kuhamasisha wanachama wapya katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.
Amesema kuwa kwa hiari yake ameacha nafasi hiyo ndani ya chama kutokana na kitendo cha viongozi wa juu wa Chama hicho kuingia ndani ya Serikali iliyopo madarakani ambayo ni ya chama pinzania kwao wao viongozi wa chini hawataweza kuwashawishi wanachama wapya kujiunga na chama hicho
Kuhusu kujiunga na chama kingine cha siasa amesema kwa sasa ni mapema mno kuzungumzia hilo kwani ataendelea kukaa pembeni na kutojihususisha kwenye mambo ya siasa huku akitafakari nini cha kufanya.
Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Wilaya ya Mbeya, Ally Mbika alisema wamepata taarifa za chini chini, lakini kama chama bado hawajakabidhiwa barua yoyote kutoka kwa kada huyo kutamka kujiuzulu rasmi.
Amesema wanasubiri kukabidhiwa rasmi ili kuweza kulizungumzia kwa vyombo vya habari barua na viongozi wa chama watapitia katiba yao na kupata mwongozo na kuangalia namna ya kuziba nafasi hiyo mpaka Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Mbika amesema kuwa kujiengua kwa kada huyo ni pigo kwa chama kwani alikuwa ana mchango mkubwa wa ushawishi na kujenga umoja na mshikamano wa kweli wa ndani na nje ya mkoa
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.