ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 8, 2017

WAZIRI MPANGO ATANGAZA KUFUTWA KWA ROAD LICENSE, SASA KULIPWA MARA MOJA.

DODOMA. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ametangaza kufutwa rasmi kwa ada ya mwaka ya leseni ya magari.
 
Amesema uamuzi umechukuliwa ili ada hii ilipwe mara moja pale gari linaposajiliwa na baada ya hapo iendelee kulipwa katika ushuru wa bidhaa  katika mafuta ya petroli na dizeli.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi bungeni na Waziri Mpango wakati akiwasilisha bajeti ya mwaka 2017/18.

 
Pamoja na hayo, Waziri Mpango ameshuha ushuru  kwa mvinyo  unaotengenezwa kwa zabibu zinazozalishwa  ndani kutoka Sh2O2  kwa lita hadi Sh200 kwa lita.

 
Kadhalika ushuru wa bia zinazotengenezwa kwa nafaka za ndani umepanda kutoka Sh429 hadi 450 kwa lita.

 
 Wakati huo, ushuru wa  bia zisizo na kilevi na vinywaji vya kuongeza nguvu kutoka Sh534 hadi Sh564 kwa lita.

Serikali yatangaza neema kwa Wafanyabiashara wadogo wadogo

Serikali imetangaza neema kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wasio rasmi wakiwamo mama lishe na baba lishe, ikiahidi kuwapa vitambulisho maalumu vitavyosaidia kuwatambua rasmi.
 
 Amesema vitambulisho hivyo vitawasaidia kutengewa maeneo maalumu ya kufanyia biashara.

 
Akiwasilisha mapendekezo ya bajeti kuu leo, Alhamisi kwa mwaka wa fedha 2017/18, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hatua hiyo inalenga kuwasaidia wafanyabiashara hao ili kukuza mitaji yao.


Usafirishaji madini wa moja kwa moja kutoka mgodini wapigwa stop

Serikali imesema haitaruhusu usafirishaji wa madini moja kwa moja kutoka mgodini na kupelekwa nje ya nchi.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi na Waziri wa Fedha na Mipango, Phillip Mpango wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti kwa mwaka 2017/18.

Badala yake kutakuwa na viwanja maalumu vya kimataifa katika bandari, migodini na madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali kabla ya kusafirishwa nje.

“Kibali hicho kitatozwa ada ya asilimia moja ya thamani ya madini hayo,” amesema.

Amesema Serikali itatangaza rasmi tarehe rasmi ya kuanza  kwa ada hiyo. 



Watumishi wa tra waonywa na Waziri Mpango

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amewaonya watumishi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) wanaowatisha na kuwazidishia kodi wafanyabiashara ili kuwakomesha, kuacha mara moja tabia hiyo.
 
Dk Mpango ameyasema hayo bungeni leo Alhamisi wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/18 na kusisitiza kwamba Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wote watakaobainika.

 
Waziri huyo amewataka wafanyabiashara kufanya shughuli zao bila hofu yoyote na kwamba Serikali inaendelea kufanya tathmini ya mwenendo wa uchumi nchini licha ya kwamba ripoti mbalimbali zinaonyesha kwamba Tanzania ina mazingira bora ya biashara.

 
“Taarifa ya Benki ya Dunia (WB) inaonyesha kwamba Tanzania ni nchi ya 132 kwa kuwa na mazingira bora ya kufanya biashara ikiwa imepiga hatua kutoka nafasi ya 144 mwaka 2015,” amesema Dk Mpango.

 
Hata hivyo, waziri huyo amesisitiza kwamba Serikali inaamini kwamba sekta binafsi ndiyo mhimili mkuu wa uchumi wa Taifa na kuwa itaendelea kushirikiana nao kuhakikisha kwamba mazingira ya biashara yanakuwa mazuri. 


 Waziri wa Fedha na Mpango Mhe.Dr.Philip Mpango akiwasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18.
 Wabunge wakisikiliza hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th Juni 2018.
 Baadhi ya wageni wakisikiliza hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th Juni 2018.
 .Wabunge wakiingia Ukumbi wa Bunge kusikiliza hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th June 2018.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.