Kwa uchache watu 14 wameuawa kusini magharibi
mwa Somalia wengi wao wakiwa ni raia baada ya kuzuka mapigano baina ya
wanajeshi wakigombea chakula cha misaada.
Taarifa zinaeleza kuwa, mapigano hayo ya kugombania chakula
ambayo mbali na kusababisha mauaji ya watu 14 yamepelekea pia makumi ya
watu kujeruhiwa yalitokea katika mji wa Baidoa ambao una makumi ya
maelfu ya raia wanaohitajia misaada ya chakula kutokana na kukabiliwa na
ukame na uhaba mkubwa wa chakula.
Mapigano hayo yalizuka baada ya baadhi ya wanajeshi kujaribu kuiba
chakula cha misaada ambapo kundi jingine la wanajeshi lilikuja na
kuwazuia wenzao hao.
Mohammed Ahmed mmoja wa maafisa katika hospitali kuu ya Baidoa
amewaambia waandishi wa habari kwamba, baadhi ya majeruhi wa tukio hilo
hali zao ni mbaya, inagawa wanaendelea kupata matibabu. Wanawake wa Somalia wakiwa katika foleni ya kusubiria chakula cha msaada
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa nchi ya Somalia inakabiliwa na ukame
na hivyo kuiongezea matatizo nchi hiyo ya Pembe ya Afrika inayokabiliwa
pia na tatizo la njaa na ukosefu wa amani na usalama.
Mbali na majanga hayo ya kimaumbile, Somalia inakabiliwa pia na
harakati za kundi la kigaidi la al-Shabaab ambalo limekuwa likifanya
mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, nusu ya raia wa Somalia
ambao ni karibu watu milioni sita na laki mbili wanahitajia msaada wa
haraka huku watoto laki tatu na elfu 63 wakikabiliwa na hali mbaya sana
ya utapiamlo.
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.