Wahisani,
mashirika ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu na serikali ya Ethiopia
wanasema kuwa, chakula cha msaada cha zaidi ya watu milioni 7.8
wanaosumbuliwa na ukame kitamalizika kufikia mwishoni mwa mwezi huu huku
nchi hiyo ikiendelea kusumbuliwa na uhaba wa misaada ya kifedha.
Uhaba
wa mvua na mabadiliko ya hali ya hewa vimesababisha ukame mkubwa nchini
Ethiopia na katika nchi nyingine kadhaa za Pembe ya Afrika. Nchini
Ethiopia pekee inakadiriwa kuwa, idadi ya watu walioathiriwa na njaa na
uhaba wa chakula itaongezeka kwa watu milioni mbili kufikia mwezi ujao.
Mwezi Machi mwaka huu Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa, njaa
iliyoyakumba maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria, Sudan Kusini,
Yemen na Somalia imesababisha mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu kuwahi
kutokea duniani tangu mwaka 1945. Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.