ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 6, 2012

OMMY DIMPOZ NA DJ ALLY WASHIRIKI PARTY YA KUZINDUA STONE CLUB MPYaaaaaaaa.......!!!!!

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz usiku wa kuamkia leo (nikimaanisha jana alhamisi) ameshiriki vyema kwenye party ya kuzindua Stone Club ambayo imekuja kivingine, na sevis mpya na wahudumu wapya  mara baada ya ukarabati wa muda mrefu. 
Party hiyo iliyokuwa ya kimya kimya ilinogeshwa na dance la nguvu lililomwagwa na Ommy Dimpoz akishirikiana na densaz wake mahiri.
Dance likiendelea katika stage ndani ya party hilo ambapo usiku huo pia ulitumika kama usiku wa kwanza mara baada ya wanavyuo kumaliza pepa.
On the one and Two alisimama Dj Ally ' mzee wa kitu juu ya kitu' toka A- town ambaye alifanya makamuzi ya hatari uspime ndani ya Stone Club Mpyaaa iliyofungwa sound full kiwango ..... Dj Ally amesaini 'kontrakti'  ya muda wa kutosha hivyo ataendelea kukisanukisha hapa.
Ommy Dimpoz kwa poz akicheza na shabiki wake mara baada ya mzuka kumpanda...

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.