ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 6, 2012

Airtel yakabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya kila siku wa Airtel Money Sabasaba

 Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kushoto) akimkabithi bwn Bernard Chezue modem baada ya kuibuka kuwa mshindi wa droo ya kila siku inayowawezesha wateja wa Airtel waliofanya malipo ya bidhaa katika viwanja vya sabasaba kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kila siku. Akishuhudia ni mfanyakazi wa huduma kwa wateja wa Airtel bi Monica Mgalwa

 Mshindi wa droo ya kila siku ya Airtel money bwana Frank Joakim Mgumba akijaribu kutumia simu yake mara baada ya kuibuka kuwa mshindi katika droo inayohusisha wateja wa Airtel walionunua bidhaa kwa kupitia Airtel money katika maonyesho ya Sabasaba. Pichani Katikati ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde pamoja na wafanyakazi wa Airtel huduma kwa wateja wa viwanja vya sabasaba.

 Mfanyakazi wa huduma kwa wateja wa Airtel bi Monica Mgalwa akichezesha droo ya kuchagua mshindi wakati wa kuchezesha droo ya kila siku iliyofanyika jana katika viwanja vya sabasaba ambapo wateja watano walionunua bidhaa kwa kupitia huduma ya Airtel money walijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo simu, modem na muda wa maongezi. Wakishuhudia pichani ni wafanyakazi wa Airtel

 Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kushoto) akimkabithi mshindi wa droo ya kila siku Bw Rucha Selemani modem baada ya kuibuka kuwa moja kati ya washindi wa siku , droo hiyo inahusisha wateja waliofanya malipo ya bidhaa kupitia Airtel money katika viwanja vya Sabasaba kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kila siku. Akishuhudia ni mfanyakazi wa huduma kwa wateja wa Airtel bi Heleni Kimati

 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Neema Academy iliyoko jijini Dar es salaam wakipata maelekezo kuhusu huduma na bidhaa mbalimbali kutoka kwa watoa huduma wa Airtel mara baada ya kutembelea banda la Airtel lililopo katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba

 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Neema Academy iliko jiji Dar es salaam wakipata maelekezo kuhusu huduma ya internet ya 3.75G kutoka kwa mfanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja baada ya kutembelea banda la Airtel lililopo katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba

Wanafunzi wa shule ya msingi ya Neema Academy iliko jiji Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea banda la Airtel lililoko katika maonyesho ya Sabasaba kilwa Road Dar es Saalam.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.