ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 6, 2012

KIMENUKA CCM WILAYA YA MISUNGWI: NI JUU YA WIZI WA ZAIDI YA SH. BILIONI 4 ZA RIPOTI YA CAG

KAMATI ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza iliyoketi leo imetoa tamko lake juu ya viongozi wa chama hicho Wilayani Misungwi kubainika kuhusika katika sakata la ubadhilifu wa fedha za Umma zilioripotiwa kupote katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa huo Saimon Mangelepaa


Akiamplyfy Exclusive jioni ya leo kwenye majira ya saa 12 hivi.. Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa huo Saimon Mangelepaa amesema kuwa kufatia ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mudhibiti wa Hesabu za serikali nchini CAG iliyotolewa Bungeni ya mwaka 2009/2012 ambapo baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo walituhumiwa kuhusika na wizi wa zaidi ya shilingi bilioni 4.

bofya hapa kumsikiliza

Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza kimekaa na kufatilia kwa umakini na kubaini baadhi ya viongozi wake kuhusika kwa ukaribu katika ubadhilifu huo akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Benard Polykap ambaye naye anatuhumiwa kuhusika katika Wizi wa fedha za umma zilizotolewa na serikali kuu kwa ajili ya maendeleo katika wilaya hiyo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Clement Mabina (kushoto) akiwa na Katibu wa CCM mkoa Bi. Joyce Masunga wakati wa kikao cha kamati ya siasa kilichotoa tamko juu ya baadhi ya viongozi wake wilaya ya Misungwi wanao husika kwenye sakata la Ubadhilifu wa fedha uliolipotiwa na CAG.
Halmashauri ya Misungwi ni moja ya Halmashauri ambazo zimetajwa katika taarifa ya CAG kuhusika na upotevu wa fedha za Umma zaidi ya bilioni 4 ambapo pia mkurugenzi wake na baadhi ya watumishi wa Idara wamesimamishwa na uchunguzi ungali ukiendelea kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.
Wajumbe Kikaoni ndani ukumbi wa CCM mkoa wa Mwanza
Hivi karibuni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Ludovick Utouh aliwaonya mawaziri wapya na watendaji serikalini kwamba ripoti zake hivi sasa zina nguvu za kusimamia uwajibikaji hivyo, wanapaswa kusimamia vyema wizara zao kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Nafikiri kuna haja ya CAG kutoa elimu. kilichotokea Misungwi ni hoja zenye thamani ya kiasi hicho na si wizi. Je Halmashauri zinapokuwa zimejibu hoja na kupunguza au kufuta wananchi wanapataje taarifa?

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.