Mechi kati ya Kombe la FA kati ya Tottenham na Bolton Wanderers ilisimamishwa ghafula baada ya mchezaji wa Bolton, Fabrice Muamba kuzimia ghafula, na kushindwa kuvuta pumzi.Madaktari walijaribu kwa dakika 10 kumfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aweze kupumua, na hilo liliposhindikana, ilimlazimu mwamuzi Howard Webb kusimamisha mchezo wakati ukiwa 1-1 katika dakika ya 41.
Muamba alizaliwa tarehe 6 Aprili mwaka 1988 mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, na aliimarika kisoka katika chuo cha vijana wadogo cha Arsenal, na akiiwakilisha England katika mechi mbalimbali, tangu zile za vijana wa miaka 16, hadi zile za wale wa miaka 21. Alijiunga na Birmingham mwaka 2007, na kuhamia Bolton mwaka uliofuata.
Tangu kufikishwa hospitali, hakuna habari zaidi zilizotolewa kuhusiana na hali yake ya afya hadi sasa.
Mambo sita kuuelewa msimamo wa Papa mpya
-
Papa Leo alichaguliwa kuwa kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki Alhamisi
kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Papa Francis, katika kongamano la siku
mbili katika...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.