ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 18, 2012

TOTO YAJISAFISHIA NJIA KUBAKI LIGI KUU YAICHAPA POLISI 2-1

Ikicheza nyumbani dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza, timu ya Toto Africans leo imefanikiwa kujikusanyia kibindoni pointi zote tatu mara baada ya kuifunga Polisi ya Dodoma bao 2-1.Toto ndiyo walikuwa wa kwanza kujipatia goli dakika 13 likifungwa umbali wa mita 35 na mchezaji Erick Mliro, hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Toto walikuwa wakiongoza 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Toto wakikosa kuzitumia vyema nafasi nyingi walizopata na walikuwa Polisi wenyebahati kwa kusawazisha dakika ya 48 kipindi cha pili mfungaji akiwa Juma Juma aliyemalizia mpira uliopanguliwa na kipa wa Toto erick Ngwenge.

Dakika ya 90 Toto walizawadiwa penati mara baada ya Christian Ramadhani kuunawa mpira ndani ya 18, bila ajizi Tete Kang'ang'a akaukwamisha kiufundi wavuni. Hadi Mwisho Toto 2, Polisi 1.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.