ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 15, 2012

GALILE VS MASHALI WATAMBIANA KILA MMOJA KUNYAKUA UBINGWA

MABONDIA Selemani Galile na Thomas Mashali wanatarajia kupanda ulingoni Aprili 9 kuwania mkanda wa ubingwa wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) litakalofanyika katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es Salaam.
Mabondia, Selemani Galile kushoto na Tomasi Mashali wakitazamana kwa usongo wa kila mmoja kutaka kuchukua mkanda wa ubingwa wa mchezo wa masumbwi wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini TPBO walipokuwa wakitambulisha mpambano wao. Dar es Salaam jana, utakaofanyika Apri 9.katikati ni Rais wa Oganaizesheni hiyo Yasin Abdallah Mwaipaya.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Pambano hilo linatarajiwa kuwa kati uzito wa kg 75 raundi 10 likiratibiwa na TPBO.
Wakitambiana Dar es Salaam jana, wakati wa kuonyeshwa mkanda huo Galile alisema atahakikisha anafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika atauchukua kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao. "Mkanda lazima niiuchukue kwani najua Mashali haniwezi na hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo najiamini na mkanda ni wangu," alisema Galile.

Naye kwa upande wake Mashali alisema raundi 10 ndio zitaamua mkanda ni wanani lakini anaimani ataunyakuwa kwani anamazoezi ya kutosha na bado ataendelea kujifua na kuhakikisha anaibuka bingwa."Ninauwezo, nimejipanga na ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote raundi 10 ndio zitaamua nani bingwa," alisema.

Upande wake Rais wa TPBO, Yassin Abdalah alisema mkanda huo ulikuwa wazi hivyo wakaamua kuwaambia mapromota ambapo alijitokeza Prospa Rweyomamu ambaye ndio ameandaa pambano hilo hivyo bingwa atakayepatikana ndio utakuwa kwake akisubiri mpinzani

Mbali ya kuwepo na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na huuzwaji wa DVD za Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi wakiwemo mabondia Lenox Lewis, Evander Holfiled, David Haye, Waldmil Klitichiko, Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roj Jones na wengine wengi zitakuwa zikisambazwa kwa ajili ya kuwapa mabondia, mashabiki na marefarii kutambua sheria na kanuni za mchezo huo Duniani ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila Super D Alisema kuwa tangia aanze kutoa mafunzo kwa njia hiyo watu wengi wameanza kuwa na uwelewa wa mchezo wa masumbwi nchini kwa kutambua sheria na mambo mbalimbali ya mchezo alisema Super D boxing Coach ambapo mpaka sasa ameweza kutoa matoleo nane tofauti ya mabingwa wa ngumi Duniani Akichanganya na mabondia wa Nchini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.