Mbunge wa Viti maalum Mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiongea na vijana wa UVCCM kwenye moja ya baraza alilohudhuria
Mbunge wa Viti maalum Mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiwa na furaha na vijana wa UVCCM mkoa wa Iringa alipokuwa mgeni rasmi kwenye moja ya mabaraza ya vijana hao.
Mbunge wa Viti maalum Mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiwa na mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa Vijijini.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge wa Viti maalum Mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve ameipongeza jumuiya ya Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kukijenga chama.
Mbunge Rose Tweve alisema kuwa vijana wamekuwa wanafanya kazi kubwa wakati wa uchaguzi na kwenye kampeni mbalimbali za serikali kama ambavyo hivi Sasa wanavyofanya kwenye SENSA.
Alisema kuwa ni muhimu Kwa Kila mwananchi kuhesabiwa katika zoezi Hilo la sensa Ili kuiwezesha Serikali kupanga bajeti Kwa usahihi Ili kufikisha maendeleo Kwa Kila mwananchi kulingana uhitaji na idadi kamili ya watu.
Katika hatua nyingine mbunge Rose Tweve alisema kuwa bajeti ya mwaka 2021/2022 imesheheni miradi mingi ya kimaendeleo kama vile barabara,elimu,afya,Kilimo na ni bajeti ambayo itasaidia kutatua changamoto za wananchi wote.
Tweve aliwaomba vijana kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo katika kila sekta hapa nchini jambo ambalo linawafanya wananchi kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.
Alimazia kwa kusema kuwa hiki ni kipindi cha uchaguzi hivyo vijana wanapaswa kugombea nafasi mbalimbali na kushiriki katika jumuiya mbalimbali ambazo zinaendelea kufanya uchaguzi ili kupata viongozi walio bora kukiongoza chama cha mapinduzi (CCM).
Mbunge huyo alifanikiwa kutembelea mabaraza yote ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa ambayo ni Baraza la UVCCM Iringa vijijini, Manispaa ya Iringa, Mufindi na kilolo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.