.
Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, wamepongeza juhudi za wanamichezo wa Tanzania wanavyoiwakilisha vyema Tanzania hasa katika mambo mbalimbali ikiwemo Michezo kama alivyofanya Bondia Francis Cheka.
Akitoa pongezi hizo mapema leo, Waziri wa Habari, Mh. Nape Nnauye aliyetembelewa ofisini kwake na bondia huyo pamoja na viongozi wa soka akiwemo Rais wa chama cha Ngumi pamoja na Promota wa bondia huyo, Waziri Nape ameelezea kuwa kadri wanamichezo wanavyofanya vizuri ndiyo wanavyoendelea kuipa sifa kemkem nchi hivyo wataendelea kushirikiana nao.
Mbali na kumpongeza bondia, Francis Cheka, Waziri Nape pia alimpongeza mdogo wa bondia huyo Francis Cheka, Cosmas Cheka ambaye naye aliambatana na msafara huo ambapo katika pambano lake naye alishinda mkanda wa WBF, kwa pointi dhidi ya mpinzani wake.
Aidha, Waziri Nape alimkabidhi cheti cha shukrani bondia, Cheka kama ishara ya kutambua mchango wake huo na kuiletea heshima Taifa kwa ushindi wake.
Bondia, Francis Cheka katika pambano lake hilo, alipigana na Raia wa Serbi anayeishi Marekani, Bondia, Geard Ajetovic ambapo katika pambano lao hilo, lililofanyika jijini Dar es Salaam, Cheka alishinda kwa pointi.
Ubingwa huo alioshinda Bondia Francis Cheka, ni Ubingwa wa Mabara unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF).
Tazama MO tv, kuona habari hiyo hapa:
Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mh. Nape Nnauye ametoa agizo rasmi juu ya matumizi ya tiketi za Kielekroniki michezoni kwa kulitaka Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kuakikisha linatumia tiketi hizo kuanzia Machi 9.2016 na kuachana na tiketi za kawaida huku akibainisha kuwa wataendelea kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu na hatua zaidi ilikuziba mianya ya udanganyifu.
Nape amebainishahayo muda huu wakati anazungumza na vyombo vya habari kuelezea suala la Michezo hapa nchini ikiwemo suala hilo la mfumo wa malipo kwa njia ya Kielekroniki ambapo awali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo la matumizi ya mfumo huo.
Akielezea suala hilo, amesema litaondoa ‘figisufigsu’ za mara kwa mara ambazo watu wamekuwa wakilalamikia mapato ikiwemo hayo ya Uwanja wa Taifa.
“Baada ya Machi 8 mwaka huu. Mechi zote zitakazochezwa uwanja wa Taifa, tiketi zote zitatumika ni zile za kieletroniki. Hii ni mara baada ya michezo yote mitatu iliyobaki ambayo TFF wanamalizia tiketi zao ambazo wamebazibakisha na zinaisha Machi 8. Safari hii tutafuatilia na kukagua wenyewe. Hatutakubali kuendelea kuvumilia hujuma katika hili.” Ameeleza Nape katika mkutano huo.
Tazama MO tv hapa kushuhudia habari hiyo:
Na Andrew Chale,modewjiblog
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.