ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 9, 2018

AU YAKANUSHA MADAI KUWA CHINA INAFANYA UJASUSI DHIDI YA AFRIKA.

AU yakanusha madai kuwa China inafanya ujasusi dhidi ya Afrika
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika amesema kuwa madai kwamba China inafanya ujasusi katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa ni uongo mtupu unaotolewa kwa shabaha ya kuvuruga ushirikiano wa pande hizo mbili.


Moussa Faki Mahamat ambaye yuko safarini nchini China amesema kuwa, ripoti iliyotolewa na magazeti ya Ufaransa kuhusu madai ya kile kilichoitwa 'ujasusi wa China' katika makao makuu ya Umoja wa Afrika, ni uongo mtupu.
Moussa Faki amesema hajui vipi ujenzi uliofanywa na China wa kituo cha mikutano cha makao makuu ya Umoja wa Afrika na kutolewa kwake zawadi kwa umoja huo kunavyoweza kuinufaisha China kijasusi. 
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi amesema katika mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwamba, kituo cha mikutano cha umoja huo mjini Addis Ababa ni nembo ya urafiki wa Beijing na Afrika na kwamba, ripoti ya magazeti ya Ufaransa ni njama za kutaka kuvuruga uhusiano huo mzuri.



Moussa Faki na Yi, Beijing

Hivi karibuni gazeti la Le Monde la Ufaransa liliaandika kuwa, wakati wa ujenzi wa makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa mwaka 2012, China iliweka vyombo vya ujasusi katika jengo hilo na kwamba, wataalamu wamegundua ujasusi huo hivi karibuni. 
CHANZO: PARSTODAY SWAHILI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.