Muonekano wa Nyumba yenye namba 1103/5 ambayo ipo katika eneo la Mafiat Jijini Mbeya , ilifunguliwa kesi namba 63 ya mwaka 2007 katika mahakama ya Wilaya Mbeya. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, imetoa siku saba kwa mkandarasi anayejenga nyumba ya serikali iliyoamuliwa na mahakama kuu kujengwa, kuibomoa baada ya kubainika kujengwa chini ya kiwango.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake , Afisa habari wa halmashauri hiyo, John Kilua, amesema ofisi
kupitia idara ya majengo ilitembelea eneo la nyumba hiyo inayojengwa kwa amri
ya mahakama kuu na kubaini changamoto mbalimbali za ujenzi.
Amesema, kutokana na changamoto hizo
wahusika wanaojenga nyumba hiyo wametakiwa kuibomoa na kuanza upya kwa kufuata
kanuni za ujenzi na kwamba zoezi la kubomolewa kwa jengo hilo la nyumb linatakiwa kufanyika ndani ya siku saba.
Nyumba hiyo yenye namba 1103/5 ambayo
ipo katika eneo la Mafiat Jijini hapa, ilifunguliwa kesi namba 63 ya mwaka 2007
katika mahakama ya Wilaya ambayo pia ilivunja ndoa ya Mhandisi Simbonea Kileo
na mkewe Gladness Kimaro na kuamuru mali za ndoa hiyo zigawanywe.
Amesema katika uamuzi huo,kileo
alipeleka ombi mahakamani na kuomba nyumba hiyo isiingie kwenye mgawanyo kwa
sababu aliuziwa kwa makataba maaalumu na Serikali na kwamba katika kipindi cha miaka
25 hatakiwi kuifanyia matengenezo yoyote yale ikiwamo kuiuza.
Hata hivyo aliyekuwa mke wa Kileo,
mtalaka Gladness Kimaro alikata rufaa mahakama kuu kupinga ombi la mumewe ,kwa
madai hakupeleka vielelezo kutoka kwa wakala wa Majengo wa Serikali (TBA)
kuonyesha kuwa nyumba hiyo ina mkataba maalumu na haitakiwi kuendelezwa kwa
miaka 25.
Baada ya Jaji Samweli Kalua kupitia
rufaa hiyo mwaka 2013, alitoa uamuzi kuwa kesi hiyo irejeshwe kwenye mahakama
ya wilaya na isikilizwe na hakimu mwingine na jambo lolote lisifanyike katika
nyumba hiyo.
Inadaiwa kuwa wakati Kileo akisubiri
kuitwa na mahakama ya wilaya kutokana na maamuzi ya mahakama kuu, ghafla mwaka 2015 aliondolewa kwa nguvu kwenye nyumba
na mtalaka wake lakini alikata rufaa.
Februari 8, 2017 Jaji Atuganile
Ngwala aliagiza kesi hiyo irejeshwe mahakama ya wilaya na ipangiwe hakimu mwingine
na kwamba kabla ya kesi ya msingi kusikilizwa walalamikiwa akiwemo
mfanyabiashara ambaye pia ni Mbunge S.H Amoni na mtalaka wa mhandisi
kileo, Gladness na madalali wawili wa mahakama kuirejesha na kuijenga upya
nyumba hiyo.
|
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.