Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akionyesha moja namba ya washindi wakati wakuchezesha droo ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti ambapo washindi 2000 kila mmoja alijishindia 1GB za SMATIKA Yatosha Intaneti. Kushoto ni ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah Hemedy na Afisa Masoko Airtel Nassoro Abubakar
Airtel yawazawadia washindi 2,000 wa promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti
Kampuni ya simu za mkokoni Airtel Tanzania leo imewazadia washindi 2,000 wa kwanza wa promosheni yaSHINDA NA SMATIKA Intaneti kwenye droo ambayo imechezesha jijini Dar es Salaam.
Promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti ilizunduliwa mapema wiki hii ambapo kuna washindi 1,000 wakila siku ambao wanajishindia bando ya 1GB pamoja na zawadi nyingine zikiwepo wakishinda simu za kisasa za smatiphone na moden.
Akiongea baada ya droo hiyo, Meneja Uhusiani Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema wateja wa Airtel 2000 wameweza kujishindia bando ya 1GB.
Kama mnvyoona hapa leo droo ya promosheni yetu ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti inafanyika kwa uwazi kabisa na washindi. Ni ya promosheni hii ni kutoa shukrani kwa wateja wa Airtel kwa kuonyesha uaminifu wao kwa kuendelea kutumia mtandao bora kabisa hapa nchini, alisema Mmbando.
Ni muhimu kufahamu kuwa mteja haitaji kujisajili kwa ajili ya promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti. Kile anachotakiwa kufanya ni kupiga *149*99# halafu changua namba 5 Yatosha SMATIKA Intaneti, hapo atanunua bando aidha ya siku, wiki au mwezi na kuwa mmoja wa washindi wa zawadi zetu kambambe, alisema Mmbando.
Mmbando aliongeza kuwa promosheni ya Shinda na Yatosha SMATIKA intaneti ilizinduliwa mwanzo mwa wiki na itakuwa ni ya siku 30 huku kukiwa na droo 3 kila wiki – Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Kwa droo za kila siku, wateja 1000 watajishindia bando ya intaneti yenye 1GB kila mmoja wakati kwenye droo kubwa kutakuwa na washindi 10 huku watano wakishinda simu za smatiphone na 5 wakijishindia moden.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.