Ni mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara (VPL) uliopigwa katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo Obrey Chirwa ameandika Hat-trick yake ya pili.
Pongezi ziende kwa mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa aliyefunga mabao matatu peke yake, huku bao lingine likifungwa na mzawa, winga Emmanuel Martin.
Kwa ushindi huo, timu ya kocha Mzambia, George Lwandamina inafikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 17 sasa ikizidiwa pointi nne tu na vinara Simba SC, ambao kesho watacheza mechi yao ya 17 dhidi ya Azam FC, iliyo nafasi ya tatu kwa pointi zake 33.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.