ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 15, 2011

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA MJINI MAGU

Bi Winfrida Chaukole akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro, vifaa vya asili ambavyo vilikuwa vikitumiwa tangu enzi na wazazi wa wazee waasisi wa taifa letu kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa MwanzaBw. Clement Mabina.

Muziki enzi za Mwalimu.

Kazi nyingine za mikono kwenye mabanda mbalimbali maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.



Wakuu wakitoka eneo la mabanda ya maonyesho.

Baadhi ya wananchi walio hudhuria sherehe ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika viwanja vya wazi wilayani Magu mkoani |Mwanza.

Ngoma za watu wa kabila la Sukuma kwenye maonyesho.

Mbina'

Ili kuboresha Elimu, jumla ya maabara 250 kujengwa kwenye kata mbalimbali mkoani Mwanza.

KISHA..
Baadae wakati maonyesho yakiendelea kongamano lafanyika wilayani humo, kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro ametoa wito kwa wenyeviti wa vijiji kusimamia vyema mali na miundo mbinu ya taifa kama vile mkongo wa mawasiliano ambapo kuna baadhi ya watu wameanza kuifukua na kuiba rasilimali zilizowekwa, vyuma vya madaraja ambapo baadhi ya watu wamekuwa waking'oa na kwenda kuuza kama vyuma chakavu pia alisisitiza suala la amani kama mhimili wa Taifa.

Kongamano hilo lililojumuisha wadau mbalimbali kama vile Wazee waliozaliwa siku ya Uhuru, Wataalam wa mashirika taasisi binafsi na za mashirika ya umma la kujadili, kutathmini na kuainisha maendeleo yaliyopatikana ndani ya miaka 50 tangu Uhuru wa Tanganyika .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.