ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 7, 2017

AUSTRIA KUPIGA MARUFUKU WANAWAKE WAISLAMU KUVAA HIJABU.

Waziri wa Mambo ya Nje na Utangamano wa Austria ametoa wito wa kupigwa marufuku vazi la stara la hijabu linalovaliwa na wanawake Waislamu katika maeneo ya umma nchini humo.
Sebastian Kurz, ambaye anatoka katika chama cha kihafidhina cha Christian Conservative People’s Party (OVP), amesema kuwa anaandaa muswada ambao ukipasishwa na kuwa sheria, wanawake wa Kiislamu nchini humo na hususan wafanyakazi wa umma kama vile walimu hawataruhusiwa kufunika vichwa vyao wakiwa kazini.
Amesema sheria hiyo itakuwa kali kushinda ile ya Ufaransa, nchi ambayo ilipiga marufuku vazi la burqa na kutangaza faini kubwa kwa wanaokiuka sheria hiyo.

Mwanamke wa Kiislamu aliyejistiri kwa mtandio nchini Austria.
Jumuiya inayotambulika ya Kiislamu nchini Austria ya IGGIO imekosoa muswada huo na kusisitiza kuwa, kuwabagua wafanyakazi wa umma kwa misingi ya dini yao ni kinyume cha sheria za nchi na ni hatua inayokanyaga moja kwa moja uhuru wa kuabudu. 
Vazi la burqa, lililopigwa marufuku katika nchi kadhaa za Ulaya
Haya yanajiri mwezi mmoja baada ya Angela Merkel, Kansela wa Ujerumani kutoa wito wa kupigwa marufuku vazi la niqab nchini humo.
Oktoba mwaka jana, Bulgaria ilijiunga na baadhi ya nchi za Magharibi kama Canada, Ubelgiji na Ufaransa, zilizopiga marufuku vazi la staha la burqa, linalovaliwa na wanawake Waislamu.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.