Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Gambia amekimbia nchi akihofiwa usalama wake.
Familia na watu wa karibu na Alieu Momar Njai, wamesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Gambia amekimbia nchi baada ya kutishiwa maisha kwa kumtangaza Adama Barrow mshindi wa uchaguzi wa Disemba Mosi mwaka uliomalizika 2016.
Hata hivyo wamesema Momar Njai hakutoa maelezo zaidi kuhusu ni nani aliyemtishia maisha na ni wapi amekimbiliaTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.