Pichani watuhumiwa watatu kati ya watano waliokamatwa wakilihudumia shamba la bangi wilayani Sengerema. |
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA
HABARI LEO TAREHE 5.1.2017
KWAMBA
TAREHE 4 /1/ 2017 MAJIRA YA SAA SITA USIKU (00:00) KATIKA MAENEO YA KIJIJI CHA
NYABUTANGA KATA YA BUKOKWA TARAFA YA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA,
ASKARI WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WATANO AMBAO NI 1. JULIUS NDALO MIAKA 80,
2. GEORGE JULIUS MIAKA 22, 3. JOSEPH JULIUS MIAKA 28, 4. MABULA JULIUS MIAKA
17, NA 5. TABU DAWA MIAKA 34 WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA NYABUTANGA, KWA KOSA LA
KUJIHUSISHA NA KILIMO CHA BHANGI KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA, AMBAPO JUMLA
YA MICHE YA BHANGI 17, 794 ILIWEZA KUPATIKANA KATIKA MASHAMBA YAO.
AWALI
ASKARI WALIPATA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA WATU
WANAOJIHUSISHA NA KILIMO CHA BHANGI KATIKA KIJIJI CHA NYABUTANGA, NDIPO MAJIRA
TAJWA HAPO JUU ASKARI WALIKWENDA MAENEO YA MASHAMBA YALIYOPO KIJIJINI HAPO NA KUKUTA MASHAMBA MAWILI YENYE UKUBWA WA
EKARI TATU YAKIWA YAMEPANDWA BHANGI PAMOJA NA MAHINDI. ASKARI WALIFANYA
OPERESHENI USIKU HUO YA KUNG’OA MICHE YOTE YA BHANGI KATIKA MASHAMBA HAYO,
AMBAPO KIASI CHA MICHE 17,794 YA BHANGI ILIPATIKANA NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA
WATU WATANO TAJWA HAPO JUU AMBAO WANADAIWA KUMILIKI MASHAMBA HAYO.
WATUHUMIWA
WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA HAPO
BAADAE WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, UPELELEZI NA MISAKO YA KUTAFUTA WATU WENGINE
AMBAO WANAJIHUSISHA NA KILIMO HARAMU CHA BHANGI BADO UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA
WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA
SHUGHULI ZISIZO HALALI AMBAZO ZINAKWENDA KINYUME NA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI,
BALI WAFANYE KAZI HALALI, LAKINI PIA ANAENDELEA KUWAOMBA WANANCHI KUTOA
USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI LIWEZA KUDHIBITI UHALIFU KATIKA MKOA WETU
WA MWANZA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.