ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 31, 2011

MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA ROBERT CUP NA MAENDELEO YA MPIRA WA KIKAPU MKOA WA MWANZA.

Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana mh. Gaudentia Mugosi Kabaka akihutubia katika maadhimisho ya MIAKA 10 ya mashindano ya Robert Cup tokea yalipoanzishwa mwaka 2001 yakiwa na lengo la kumuenzi marehemu Robert Chacha Kabaka aliyekuwa mmoja kati ya waanzilishi wa timu ya mpira wa kikapu ya Butimba Spiders na pia mdau mkubwa wa mpira wa kikapu hapa mkoani.

Mgeni rasmi akiongozwa na Uongozi wa MRBA kukagua timu zilizochuana.

MRBA imekuwa na mpango madhubuti ya kuinua na kuvumbua vipaji kwa kuendesha mashindano ya shule za sekondari kuanzia mwaka 2003 hadi leo.

Chimbuko la mashindano ya Robert Cup lilianzia katika uwanja huu wa chuo cha Ualimu Butimba.

Game likiendelea.

Kaimu Mwenyekiti Sosho Kizito.
"MRBA imetoa Viongozi mbalimbali ngazi za juu kama vile Mama Angelina Mabula mwenyekiti wa hazina Taifa, Mussa K. Mziya Rais wa shirikisho la mpira wa kitapu huku mama Angelina Mabula aliteuliwa tena kuwa mkuu wa Wilaya ya Muleba mwaka 2010"

Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana mh. Gaudentia Mugosi Kabaka akimkabidhi Kamishna wa Fiba International, Certificate of Appreciation.

Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana mh. Gaudentia Mugosi Kabaka akimkabidhi Mwanahabari wa Star Tv Jackob Markus, Certificate of Appreciation.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.