NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Yapo mambo ya kijamii ambayo sisi sote tunatakiwa kuungana katika kuyapiga vita na kuyatokomeza kabisa. Mojawapo ya mambo hayo ni mauaji yawatu wenye albinism, ambayo yamekuwa yakiendelea hapa nchini. Hali hii, ambayo sio tu inalitia aibu taifa letu la Tanzania, pia ni ukosewaji mkubwa wa haki za binadamu. Ukichunguza kwa undani kisa kikubwa inasemekana ni imani za kishirikina na kutafuta “utajiri” wa haraka, jambo ambalo ni imani potofu zisizo kuwa na ukweli hata chembe. ....................................................................................................................... HABARI KAMILI SERIKALI imeahidi kufanya jitihada na uchunguzi wa kina kubaini watu waliotekeleza mauaji ya mwanakijiji Joseph Msongoma (49) mkazi wa kijiji na Kata ya Ngula wilayani Kwimba mkoani Mwanza, ambaye ana ulemavu wa ngozi (ualbino) ameuawa kikatili kwa kukatwa na panga huku wauaji wakiondoka na mkono wake wa kulia. Taarifa zinasema tukio hilo lilitokea Jumatano Novemba 2, 2022 saa 4 Usiku baada ya watu hao kufika nyumbani kwa Joseph na kumwita jina lake kisha kumkata mkono wake wa kulia na kutokomea nao kusikojulikana. Mbele ya waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu Joseph, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima anatoa tamko kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza kuhakikisha waliohusika katika tukio hilo wanakamatwa.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.