Mwenyekiti wa vyama vya magonjwa yasiyoambukiza (TANCDA) profesa Andrew Swai akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya magonjwa yasiyoambukizaWaandishi wa habari wakifuatilia mafunzo ya magonjwa yasiyoambukiza
Kuelekea wiki ya Maadhimisho ya magonjwa yasiyoambukiza yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza kuanzia Novemba 5 hadi 12 mwaka huu Waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Kanda ya ziwa wamepewa semina juu ya magonjwa hayo.
Semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Afya imefanyika leo Jumatano Novemba 2,2022 Jijini Mwanza.
Akizungumza katika semina hiyo Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya afya Shadrack Buswelu, amesema lengo la kuaandaa mafunzo hayo ni kuwawezesha waandishi wa habari kutoa taarifa ambazo ni sahihi kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza kwenye jamii sanjari na kuwaelimisha ili waweze kuchukua hatua madhubuti za kujikinga dhidi ya magonjwa hayo.
Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyoambukiza Tanzania (TANCDA) Prof. Andrew Swai, amesema magonjwa yasiyoambukiza yanaenea kwa wingi ikiwemo kisukari, Saratani,magonjwa sugu ya njia ya hewa,kuoza meno, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, na magonjwa ya akili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.