ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 1, 2022

DAVIDO APOTEZA MTOTO KWA KIFO CHA UTATA.


 Ni siku ya huzuni kwa mwanamuziki Davido na mchumba wake, Chioma Rowland, baada ya kumpoteza mtoto wao wa kiume, Ifeanyi Adeleke. 

Mwanawe Davido anasemekana kuzama kwenye bwawa la kuogelea bomani kwao katika kisiwa chao cha Banana, Lagos, Nigeria, Oktoba 31. 

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, mtoto huyo wa miaka mitatu alipatikana akiwa amepoteza fahamu kwenye bwawa la kuogelea na kukimbizwa katika hospitali ya Lagos, ambapo alitangazwa kuwa amekata roho. 

 Davido na Chioma walikuwa mbali katika Jimbo la Ibadan kwa mkutano wa familia msiba ulipotokea. 

Habari za kusikitisha zilienea kwenye mitandao ya kijamii, na Kamanda wa Polisi wa Jimbo la Lagos, Benjamin Hundeyin, alithibitisha kifo cha mtoto huyo wa miaka mitatu. Kulingana na ripoti ya BBC Pidgin, mmoja wa wafanyakazi wa nyumbani wa Davido alipiga ripoti kuhusu tukio hilo lililotokea Jumatatu usiku katika kituo cha polisi cha eneo hilo. 

Kufikia sasa, wafanyikazi wanane wa mwimbaji huyo wamehojiwa na polisi. 

AY Comedian alisema: "Kifo cha mtoto si cha kawaida, si cha haki na ni cha kusikitisha. Hii imeniuma sana." Naviomusic alisema: "Pole kwako, kaka yangu @davido. Mtoto Ifeanyi Apumzike Kwa Amani." 

Steflon Don alisema: "Nawaombeeni dua Chioma na Davido ❤️." 


Nyota huyo wa muziki alisherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe wa pekee wa kiume mnamo Oktoba 20, 2022, kwa ujumbe mtamu. "Nakuombea kwa moyo wangu wote Mungu akupe afya njema na furaha tele kwa muda wote uwezavyo kibinadamu. 

Utakuwa na mafanikio makubwa kuliko yangu Happy birthday, son @davidifeanyiadeleke !!! #BIG3 ," alichapisha ujumbe huo akisindikiza na picha murwa za bingwa huyo mdogo. 

Akisherehekea tunda la kwanza la tumbo lake la uzazi, Chioma aliandika ujumbe mtamu kwake Ifeanyi, na akasema: “Happy birthday mpenzi wa maisha yangu. Mama anakupenda sana, Mungu akujalie mema siku zote. 

Mungu amekuwa mwaminifu sana kwetu na nashukuru sana kuitwa mama yako. Nakutakia mafanikio makubwa zaidi ya wazazi wako. katika jina la Yesu, amina. Nakupenda pacha wangu." 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.