NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
OMBI limetolewa na wakazi wa Zenze kata ya Kiseke wilayani Ilemela jijini Mwanza baada ya baadhi ya wananchi kudai kutoshirikishwa katika elimu kuhusu uelewa wa upandaji wa miti ikiwemo oparesheni ya ukataji wa miti jirani ya miundombinu ya shirika hilo. Mwenyekiti wa mtaa wa Zenze Shija Ndungile ni mmoja kati ya wananchi walioathirika na oparesheni ya ukataji wa miti katika makazi yake, amesema kuwa wakati zoezi hili likitekelezwa na Tanesco hapakuwepo na elimu wala taarifa yoyote inayoashiria utekelezaji wa zoezi hilo. Kupata ufafanuzi kuhusu oparesheni hiyo Jembe Fm imebisha hodi katika ofisi za Shirika la Umeme Tanzania Tanesco mkoa wa Mwanza kuzungumza na meneja wa Shirika hilo Mhandisi Said Msemo naye akafunguka. Shirika la umeme Tanzania Tanesco linaendelea na oparesheni ya ukataji wa miti iliyopo jirani na miundombinu ya umeme katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza ili kulinda usalama wa maisha ya wananchi.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.