ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 5, 2018

NI MOHAMED SALAH TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA 2017


Mohamed Salah amempiku mchezaji mwenzake wa Liverpool, Sadio Mane na mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang kutwaa Tuzo ya Mchezaji wa Afrika wa Mwaka 2017.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri aliibuka mshindi katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya wachezaji wenzake katika mkutano wa Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika mjini Accra.

Salah, ambaye ataikosa mechi ya Kombe la FA raundi ya tatu dhidi ya Everton, Ijumaa usiku, amefurahia mwaka wa mafanikio kwa klabu na kwa taifa lake pia.

Baada ya kufunga mara 10 akiwa Roma kati ya Januari na Mei, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aijiunga na Liverpool kwa uhamisho wa rekodi kwa klabu hiyo na kwa haraka ameshafanikiwa kuweka kimiani magoli 24 katika michuano yote.

Akiongea kuelekea hafla hiyo, Salah aliwaambia waandishi: “Nadhani tuna timu bora ya taifa na tumefanya vizuri kwenye Kombe la Afrika na kufuzu Kombe la Dunia.”

Salah pia alizifumania nyavu mara mbili katika ushindi wa Misri wa 2-1 dhidi ya Congo kufuzu Kombe la Dunia Oktoba kuhakikisha timu yake ya taifa inapata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 28.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.