Wateja wa Airtel sasa kutuma SMS kwa
Shilingi Moja
· Ujumbe mfupi utatozwa shilingi 1 badala ya shilingi 54 kwa sms
· Sms kwenda mtandao wowote nchini
3
January 2013, Airtel Tanzania kampuni ya simu
inayoongoza kwa mtandao mpana na huduma bora na bei nafuu leo imetangaza bei
mpya yenye punguzo la gharama za kutuma ujumbe mfupi ili
kuwapati wateja wake urahisi na unafuu wa huduma ya ujumbe mfupi nchini. Airtel
imepunguza gharama za sms kutoka shilingi 54 hadi shilingi 1 kwa
kila sms.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa gharama mpya ya sms Meneja bidhaa na masoko Francis
Ndikumwami alisema” Leo tunayofuraha kuzindua SmS Kichizi ofa ya peeke itakayowawezesha wateja wa Airtel
kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa gharama nafuu. hii
ni ya kwanza kutoka Airtel ambapo tumewapatia na kuwawezesha wateja wetu nchi
nzima kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa gharama nafuu ya shilling 1 kwa kila ujumbe
mfupi kwenda kwenye mtandao wowote masaa 27 siku 7 za wiki bila kikomo. sasa
wateja wa Airtel watatozwa shilling 125 kwa ujumbe wa kwanza wa sms na zingine
zitakazofuata zitatozwa gharama ya shilling moja kwa siku”.
“SMS
kichizi huduma ya ujumbe mfupi ni mwendelezo wa kutimiza dhamira yetu ya kutoa
huduma bora, kuwapa wateja wetu uzoefu wa pekee katika huduma zetu za wateja na
kutoza gharama nafuu. Airtel leo ndio mtandao ulioenea zaidi maeneo mengi
nchini na kuwafikia watanzania wengi zaidi kupitia huduma zetu za Airtel money
na internet yenye kasi zaidi nchini.” aliongeza Ndikumwami
Gharama
hizi mpya za ujumbe mfupi zitatozwa kwenda mitandao ya ndani ya nchini tu na
ni kwa wateja wa Airtel wa malipo ya awali nchini.
Akiongea
kuhusu muda wa huduma hii Francis Ndikumwami alieleza, Airtel tunawajali wateja
wetu hivyo huduma hii ya SMS Kichizi sio promosheni ni huduma ya kudumu.
Airtel
bado inaendelea na promosheni yake ya msimu wa sikukuu ya Amka millionea ambapo
wateja wengi nchini nzima wameendelea kujishindia pesa taslimu ambapo wateja
zaidi ya 300 wameshajishindia jumla ya pesa taslimu zaidi ya shilling million
120 hadi sasa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.