ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 3, 2013

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA ILEMELA LAENDELEA KUKUMBWA NA MTAFARUKU KWA MADIWANI WA CHADEMA KULISUSIA, KIKAO CHAENDELEA, MEYA ASISITIZA MSIMAMO WAKE WA KUTOWATAMBUA MADIWANI WA3 ALOWATIMUA.

Meya wa Manispaa ya Ilemela ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangili, Bw. Henry Matata akitoa ufafanuzi ndani ya kikao cha baraza la madiwani kilicho fanyika leo jijini Mwanza na kuhusisha pia na wataalamu wa vitengo mbalimbali na idara zake wa wilaya hiyo .

Na. ALBERT G. SENGO: MWANZA
BARAZA la Madiwani wa Manispaa ya Ilemela limendelea kukumbwa na mtafaruku kwa Madiwani wa Chama cha CHADEMA Wilayani humo kuendelea na msimamo wao wa kutomtambua Meya  Bw. Henry Matata (CHADEMA) ambaye ni Diwani wa Kata ya Kitangiri na kususia kikao cha Baraza hilo kilichofanyika leo katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo eneo la Busweru jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw. Zubery Mbihna mara tu alipomaliza kuwasilisha ajenda saba za kikao hicho Diwani wa Nyakato Bw.Josephat Manyerere (CHADEMA) alinyanyuka na kutaka ajenda ya Maswali na Majibu iwe ya kwanza kujadiliwa na Chama Chake  kiwe cha kwanza kuwasilisha maswali yake iliyokuwa imeyaandaa hali iliyoleta mabishano makali na kelele za malumbano hali iliyopelekea  Madiwani wote wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi.

Hata hivyo Meya Bw. Matata kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria zilizopo za Halmashauri hiyo aliwatuliza wajumbe waliosalia wakiwemo wataalaamu kisha akatangaza kuendelea na ajenda kama zilivyo wasilishwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Madiwani.

Kufuatia mtafaruku huo uliopelekea Madiwani wa CHADEMA kutoka na kususia kwa mara nyingine kikao cha baraza, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ananini cha kusema juu ya hali hiyo na hali hii ya kutokukubalika na madiwani wenzake wa CHADEMA anaichukuliaje… BOFYA PLAY MSIKILIZE


Licha ya kusaini kitabu cha mahudhurio na kususia kikao hicho, madiwani hao wa CHADEMA baadaye walionekana wakiingia kwenye chumba cha mhasibu wa Manispaa ya Ilemela na kuchukuwa posho zao za kuhudhuria kikao hicho cha kujadili masuala ya maendeleo.
Naibu meya wa Manispaa ya Ilemela Bw. Dede Swila (CCM) akichangia hoja kwenye kikao hicho ambacho kilianza na zengwe pamoja na makeke mengi lakini kiliisha kwa salama.

Taswira ya kikao toka juu.

Wataalamu na wafanyakazi wa idara mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya kikao hicho.

Diwani wa kata ya Buswelu Thobias Mpemba akichangia hoja kati ya ajenda zilizo wasilishwa.

Afisa habari wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela Bi. Viola (kushoto) akiwa na ameketi meza moja na wataalamu na wafanyakazi wa idara mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya kikao hicho.

Mtaalamu wa moja kati ya vitengo wilaya ya Ilemela akitoa ufafanuzi kwamoja ya hoja zilizowasilishwa. 

Mtaalamu.

Mkuu wa wilaya ya Ilemela.

Meya wa Manispaa ya Ilemela ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangili, Bw. Henry Matata mara baada ya yaliyojadiliwa kufikia tamati katika uwasilishwaji na kutolewa ufafanuzi aliahirisha kikao hicho kilichohudhuriwa na madiwani na kuhusisha wataalamu wa vitengo mbalimbali na idara zake toka wilayani humo.

Jengo la Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.