ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 1, 2026

DKT. MWIGULU ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI NJOMBE


WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Mei 1, 2026, ameshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika mkoani Njombe.

Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Akizungumza katika maadhimisho hayo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu ametoa wito kwa wafanyakazi wote nchini kuwa wavumilivu na kuto kata tamaa katika majukumu yao ya kazi ili kufikia mafanikio ya pamoja.


Kadhalika, Dkt. Mwigulu amewaasa waajiri kujenga mazingira chanya yatakayowafanya wafanyakazi wajisikie kuthaminiwa, jambo linalosaidia kuongeza mshikamano na ustahimilivu wa kiutendaji.


Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa: “Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.”




Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment