ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 27, 2026

UWANJA WA BENJAMIN MKAPA KUKAMILIKA MIEZI SITA IJAYO.

Uwanja Benjamin Mkapa kuboreshwa kisasa

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ametangaza kuanza kwa maboresho makubwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Msigwa amesema maboresho hayo yanahusisha sehemu ya kuchezea (pitch), ambayo inatarajiwa kufikia viwango vya kisasa ndani ya kipindi cha miezi sita.

Ameeleza kuwa lengo ni kuwa na uwanja wenye viwango vya kimataifa, sambamba na kuboresha maeneo mengine ikiwemo sehemu za wageni maalum (lounges), vyumba vya kubadilishia nguo, ubao wa matokeo pamoja na mwonekano wa jumla wa uwanja.

Aidha, ameomba radhi kwa mashabiki wa soka kwa kutoweza kuutumia uwanja huo katika dabi ya Kariakoo iliyopangwa kufanyika Mei 3, 2026.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa baada ya maboresho kukamilika, uwanja huo utakuwa katika hali bora zaidi na utadumu kwa matumizi ya muda mrefu.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment