Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti
wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipofika
kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji
,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti
wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia (wa kwanza kushoto waliokaa) akiteta jambo na Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Naibu waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha wakati walipofika kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akikata utepe tayari kwa uzinduzi wa kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Kutoka Kushoto (mwenye suti bluu) ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Sailesh Pandit, Mwenyekiti wa kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia wakiongozana na Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti
wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akimkaribisha Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuongea na hadhara iliyopo kwenye kiwanda hicho mara baada ya
kuzindua kiwanda kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea machache mara baada ya
kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akizindua jiwe la msingi katika kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Sailesh Pandit akiagana na Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya
kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo
Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa kampuni
ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akiagana na Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya
kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo
Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Sailesh Pandit akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi ambaye niWaziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya
kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo
Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016. Picha zote Gadiola Emanuel
habari na Woinde Shizza , Arusha.
Halmashauri za majiji, manispaa na miji
wametakiwa kutumia mabomba ya maji yanayozalishwa nchini badala ya kuagiza
bidhaa hiyo toka nje ili kuweza kuvinufaisha
viwanda vya ndani.
Hayo
yamebainishwa na waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim
Majaliwa
wakati akizindua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya Plastic ya maji
yenye ukubwa wa aina mbalimbali (Lodhia Plastics ) kilichopo njiro
jijini
hapa.
Alisema
kuwa haiana haja ya halmashauri au
majiji kuagiza bidhaa mbalimbali nje ya nchi
wakati nchi yetu inaviwanda vya
kutosha vya kutengeneza bidhaa hizo.
“Sioni
sababu ya wahandisi wa Halmashauri na washauri elekezi halmashauri kushinikiza
wakandarasi wa hapa Arusha kwenda kununua mabomba ya maji nje ya mkoa wakati
hapa kuna kiwanda kama Lodhia ambacho kinatengeneza hizo bidhaa kwakweli hii
labda iwe ni chuki tu”alisema Majaliwa ambaye ameanza
ziara ya siku nane mkoani Arusha.
Alisema
ni muhimu kwa halmashauri kununua mabomba hayo kwa matumizi ya miradi ya maji
na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wawekezaji wa ndani.
“Washauri
wa miradi mbalimbali acheni chuki …waache wakandarasi wanunue bidhaa bora
zilizothibitishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TBS) na Shirika la Viwango la
Kimataifa (ISO),” alisema.
Aidha
alitoa mfano, kwa upande wa Mkoa wa Arusha kuna mpango wa kujenga mradi mkubwa
wa maji utakaogharimu dola za Marekani milioni 200, na katika utekelezaji wake
ni lazima watoe kipaumbele cha kutumia mabomba yanayozalishwa na kiwanda hicho.
Mradi
huo ukikamilika unatarajiwa kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa jijini hapa.
Alisisiza
haoni umuhimu wa halmashauri na wakandarasi kununua mabomba kutoka nje ya
Arusha au nje ya nchi wakati kuna mabomba yanayozalishwa na wawekezaji wazawa
na yanakidhi viwango.
“Serikali
yetu itaendelea kuwaenzi na kuwalinda
wawekezaji wote wa ndani ambao wamekuwa msaada mkubwa wa kutoa ajira ambayo ni
janga kwa taifa na dunia kwa ujumla”alisema Majaliwa.
Awali
Mwenyekiti wa Bodi ya Lodhia Group, Arun Lodhia, alisema serikali ichukue
nafasi ya kuzungumza na wenye viwanda mara kwa mara ili kujua matatizo yao na
kuyatafutia ufumbuzi.
Alisema
viwanda chini ya kampuni hiyo, vinazalisha bidhaa nyingi zenye ubora lakini
makampuni yanashindwa kununua na kupenda zaidi kununua bidhaa za nje.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Sailesh Pandit, alisema kwamba wanashindwa kuuza mabomba ya maji na
malighafi nyingine katika miradi mikubwa ya maji iliyopo mkoani Arusha.
Alisema
wanashindwa kufanya hivyo licha ya bidhaa zao kuwa na TBS na ISO kutokana na
hujuma wanazofanyiwa na baadhi ya wahandisi na washauri elekezi wa miradi.
“Imeshatokea
mara kadhaa kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi kuzuiwa kununua mabomba ya
maji kutoka Lodhia Plastics na badala yake hulazimishwa kununua mabomba kutoka
nje ya mkoa hivyo kuwasababishia gharama za ziada,” alisema.
Kuhusu
ajira, alisema kiwanda hicho kimetoajiri Watanzania kati ya 1, 200 hadi 1, 300 lakini
pia Watanzania zaidi ya 500 wananufaika kutokana na kushiriki katika utoaji wa
huduma mbalimbali kiwandani hapo.
Alisema
mtandao wa viwanda vinne vinavyomilikiwa na kampuni ya Lodhia Group wanalipa kodi
wastani wa Sh. bilioni 20 kwa mwaka.
Kwa
upande wao, baadhi ya makandarasi, Samuel Lugemalila wa Kampuni ya Vest
Tanzania Ltd na Kastuli Mandange kutoka Fraju Group Ltd na Maxmilian Iranghay wa kampuni Wining Spirit Construction Ltd,
walitoa ushuhuda kuhusu namna washauri waelekezi na watumishi wengine
wanavyowakataza kununua bidhaa za Lodhia Plastics na kuwataka wanunue
zinazotengenezwa nje ya mkoa.
Walisema
kitendo hicho kinawashababisha kushindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati na
kuwaongezea gharama kubwa.
Aidha
waliiomba serikali kuondoa urasimu kwa wahasibu kulipa malipo kwa wakati licha
ya miradi kukaguliwa na kupata cheti cha uhakiki wa kazi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.