Zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo kutoka katika maeneo yasiyoruhusiwa katikati ya jiji la Mwanza imefanyika kwa ufanisi kufuatia jeshi la polisi kwa kushirikiana na mgambo kufanya operesheni bomobomoa katika eneo la makoroboi na Tanganyika usiku wa kuamkia leo la kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya jiji.
wakizungumza na vyombo vya habari jijini Mwanza Wakuu wa wilaya za Nyamagana na Ilemela wamesema zoezi la kuwapanga wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama machinga katika maeneo mapya Nyegezi, Kiloleli na Buzuruga linaendelea.
Hii ni moja ya operesheni zilizofanywa na Mgambo wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kukamilika kwa ufanisi mkubwa katika kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama machinga kutoka katika maeneo yasiyoruhusiwa katikati ya jiji.
Operesheni hii ya kuwaondoa watu wanaofanyabiashara katika maeneo yasiyoruhusiwa ilianza usiku kwa kuwakamata wanawake wanaofanya biashara ya ngono na wazururaji, na baadaye kufanya bomoa bomoa katika eneo la makoroboi na Tanganyika na mtaa wa soko kuu, maeneo ambayo ni shughuli nyingi jijini.
Zephania Mandia wa gsengoblog.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.