ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 20, 2016

MAJAMBAZI 8 WASHIKILIWA NA POLISI MWANZA.

Kamanda Ahmed Msangi.




NA. ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza

JESHI la polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watu nane wanaosadikika kuwa ni majambazi katika matukio mawili tofauti waliofanya uhalifu wa unyang’anyi wa mali pamoja na wizi wa gari.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoani hapa Ahmed Msangi leo, amesema kuwa kwenye tukio la kwanza wamefanikiwa kukamata watu sita  wakiwa na silaha mbili  za kienyeji zikiwa na risasi 23 ambazo zilikuwa zikifyatuliwa juu na kufanya unyang’anyi.

Tukio hilo limetokea Oktoba 18 saa 7 mchana huko maeneo ya buswelu Wilaya ya Ilemela Mkoani hapa  ambapo walipora fedha 35,000 na mali ambazo hazijajulikana.

“Watu tuliowakamata ni Jeremiah Marigia(Mkumbo)(25) mkazi wa Singida ambapo alitoka kwenye Mkoa huo kwa ajili ya kufanya uhalifu Mwanza na tulipomuhoji alikiri kufanya vitendo hivyo na kuwataja wenzake watano kuwa wanazo silaha na wanazitunzia kwa mganga wa kienyeji na tulipoenda kweli tuliwakuta na kuwakamata lakini kwenye tukio hilo hakuuwawa mtu yeyote”amesema Msangi.

Siku hiyo hiyo  saa 8 mchana Watu wawili Rahim Feka (28) na Ally Kahalale(32) wote wakazi wa jiji la Dar-es-salaam wamekamatwa na jeshi hilo wakiwa na gari la wizi T 778AZB aina ya Land cruiser liloibwa Manispaa ya Ilala Mkoani humo  kwa ajili ya kuliuza jijini hapa.

Kamanda amesema kuwa gari hilo limepatikana Buzuruga baada ya jeshi hilo kufanya upelelezi kufuatia taarifa walizozipokea kutoka Dar-es-salaam kuwa kuna wizi wa gari hilo na huenda limeletwa Mkoani Mwanza.

“Hawa watu bado tunaendelea kuhojiana nao yawezekana wana mtandao unaofanya kazi za kuiba magari kutoka huku Mwanza na kuyauza Dar au kuiba Dar na kuyuza mikoa mingine kwa hiyo wananchi tuwe makini na vitu vya wizi kwa sababu gari haliuzwi kama bakuli mnadani na baada ya mahojiano tutawapeleka Dar ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliw dhidi yao”amasema Msangi. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.