ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 13, 2011

"UKITOKA KAZINI TUPITIE SOKO LA JIONI...."

Mara baada ya halmashauri ya jiji la Mwanza kutoa ruksa kwa wafanyabiashara ndogondogo kufanya biashara zao jioni katika maeneo yaliyotengwa, zoezi hilo limeonekana kuwanufaisha wengi kwa kuwarahisishia upatikanaji wa bidhaa mbalimbali za majumbani pamoja na chakula.

Samaki wa kukaushwa aina ya sangara maarufu kwa jina la 'vibambala' wakiwa katika hali hii wanauwezo wakukaa muda mrefu bila kuharibika ikiwa tu watahifadhiwa vyema kulingana na kanuni zake, ladha tamu ukipika kwa nazi.

Dadaa, samaki wabichi, mihogo, viungo na viazi aina zote vinapatikana hapa.

Sehemu ya mboga mboga mbele kabisa kuna mahala pa mitumba na bidhaa za machinga. Eneo hili limekuwa kiungo kurahisisha mahitaji kutokana na kuwa katikati ya mji, upatikanaji wa bidhaa mbalimbali na usafiri wa daladala kwenda maeneo yote ya ndani na nje ya mji kuwa karibu na eneo hili la soko.

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Duh! nimetamani kweli, mate hayo yanadondoka ovyo ovyo...

    ReplyDelete
  2. Aluu samaki hawa wakikutana na mpishi mzuri kama mie mwenye mkono, mbona utapenda, hongera sengo kwa kutuletea vitu different.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.