Ile michuano ya Fiesta Soka Bonanza mara baada ya kufanyika jijini Dar es salaam kwa msisimko na mvuto wa aina yake na mwisho wa siku ikishuhudiwa mashabiki wa Real Madrid wakafanikiwa kunyakuwa kombe na kitita cha shilingi milioni moja nao Chelsea wakiambua nafasi ya pili na kunyukwa kitita cha shilingi laki tano, sasa michuano hiyo kufanyika Mwanza katika dimba la CCM Kirumba tarehe 23 April 2011.Mratibu wa michuano hiyo jijini Mwanza Albert G. Sengo amewataka viongozi wa kujitolea wa timu hizo (marais) kuwasiliana nae au kufika katika ofisi za Clouds fm Mwanza 88.1 zilizopo jengo la CCM mkoa ghorofa ya tano au kwa simu no +2550754074152 kwaajili ya kutoa mwongozo kwamba ni maeneo gani ya kukutana mashabiki kwaajili ya kuboresha ushangiliaji na kutengeneza timu.
Aidha G. amesema kuwa timu nzima ya watangazaji wa Sport Extra inataraji kutua Mwanza siku ya jumapili kwaajili ya matayarisho na mchakato mzima kuelekea siku ya michuano.
Shukurani kwa Starmax Hotel kwa kudhamini wageni wa kipindi cha michezo Clouds fm.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment