ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 13, 2011

WABUNGE KWA MWENDO HUU SIKU SI NYINGI MTACHAPANA VITI..YAaaNI NAVIONA KABISA ..!!

Niliidaka juu kwa juu tu! leo katika mjadala wa kupitisha Hoja moja wapo kuelekea mchakato wa kupata wawakilishi wa Bunge la Afrika kupitia televisheni LIVE na nikakuta Mbunge wa Nyamagana Mh. Ezekiel Wenje ndiye alikuwa amesimama akitoa pendekezo nao wabunge wenzake wakimzodoa.
Mara sauti zikasikika na nilizozinasa ni hizi;

*****-"akanywe kikombe cha babu huyo...!"
*****-"futa kauli!"
*****-"we vipi waambiwa huna maskio!"
*****-"jamani hatuko klabu tuko bu-nge-ni!"
*****-"out!out katuburuza huyo!!"

SPIKA: "jamani naomba utulivu!!"

*****-"hatoki mtu nje!!"
*****-"tutatoka wote....!!!"
*****- "tufunge mlango tupigane!!...!!"
(***)-"naona mnafanya mnada badala ya kuendelea na bunge"
*****-"msitumie wingi wenu kutuburuza!!"

SPIKA: "watu mmechaguliwa na kura za wananchi kwanini mwafanya mambo ya kitoto hivi hamjui kuwa tunaonwa na wananchi?...!

Ndipo atilisti utulivu ukapatikana uchaguzi wa Pan Africa Parliament ukaendelea....

Tupe maoni yako

3 comments:

  1. Wabunge Kuzipiga siyo kitu cha ajabu sana; wangeacha zipigwe tu;
    Wenzetu Kenya kama mambo yanapelekwa ndivyo sivyo uwa apatoshi.

    Safi wapinzani!
    Bado la Katiba na Dowans

    ReplyDelete
  2. Ukiangalia vizuri bunge hili linavyoendeshwa utagundua Spika Makinda anashindwa kuliongoza Vyema hilo bunge, wabunge wa CCM wanatumia ubabe wa wingi wao kupayuka.
    Mabaraza ya maamuzi ya Ugiriki ya kale Ancient Greece Senate(Bunge ukipenda kuliita hivyo, maamuzi yalifikiwa kwa kungalia nani aliongea kwa sauti kubwa zaidi na si nani alitoa hoja bora zaidi. Spika Makinda na kundi lako la Wabunge wakora wa CCM, (na baadhi ya wabunge wa upinzani) msilifanye bunge la Tz kuwa kama soko.
    Watnzania wana matatizo mengi ya msingi, wabunge wanaishia kupigana vijembe...!!!
    Mnajalia kweli ustawi wa watu wenu???

    ReplyDelete
  3. Wananchi tuamke tuache ushabiki, wabunge wote wanatuibia tu! hivi unajua kwa mwaka wanatia mifukoni mabilioni mangapi? Ni zaidi ya epa na richmond, halafu miaka mitano ikiisha hakuna tofauti yeyote, tuwakatae wote bajeti inayotengwa kuhudumia bunge kwa miaka mitano inaweza kusaidia nchi hii kupunguza umaskini kwa asilimia kubwa tu. Vipi kama likikaaa kila baada ya miaka miwili halafu zile pesa za vikao tukazifanyia mipango iliyosimama? tutafika mbali..

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.