Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakitengeneza vitabu vya hesabu ili kukwepa kupeleka kodi kubwa ya ongezeko ya thamani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Amesema linapofika suala la kuwasilisha asilimia 18 ya VAT wengi wamekuwa wakibaki nayo kama mtaji badala ya kuipeleka serikalini huku akibainisha wamekuwa wakitengeneza vitabu tofauti.
“Kimoja ni cha benki chenye mahesabu ya kweli yenye faida na kitabu kingine ni cha TRA. Kwa kawaida kile kinachopelekwa benki kinakuwa cha kweli lakini kinachoenda TRA ni kidogo wakati mwingine kinaonyesha hasara,” amesema Rais Magufuli leo katika mkutano kati yake na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini unaojadili changamoto wanazokutana nazo na kuzitafutia majibu.
“Nataka nitoe mfano wa kampuni tatu, moja ya kampuni (Jina linahifadhiwa) ina vitabu vitatu na fedha zake ni hatari ukiangalia, nina uhakika huyo mfanyabiashara ataenda akairudishe hiyo hela iliyokuwa inatakiwa,” amesema Rais Magufuli .
“Kampuni nyingine namba mbili (Jina linahifadhiwa) taarifa ya benki inaoyesha mwaka 2017 inaonyesha faida ilikuwa Sh958 milioni lakini iliyopelekwa TRA ni Sh20 milioni kwenye kitabu cha pili, kampuni namba tatu mwaka 2017 taarifa ya benki inaoyesha faida ilikuwa Sh501 milioni lakini TRA iliambiwa kuwa imepata faida ya Sh72 milioni.”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.