Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, na kila mzazi hufurahia kuona watoto wake wanaishi katika mazingira mazuri yanayowawezesha kupata haki za msingi na kuwa raia wema katika kulitumikia taifa na kuleta maendeleo katika vizazi vijavyo.
Watoto wanatakiwa wajisikie salama wakiwa nyumbani, shuleni na kwenye jamii inayowazunguka. Lakini katika maeneo mengi ukatili dhidi ya watoto hufanyika na wakati mwingine kutoka kwa watu ambao wanawaona kila siku. Kwa watoto wengi suala la kufanyiwa ukatili linaonekana zaidi katika sura ya kifamilia.
Suala ukatili dhidi ya watoto linatokea kila mahali kwa sura tofauti tofauti kulingana na mazingira anayoishi mtoto. Hata kwenye nchi ambazo zimepiga hatua kubwa ya maendeleo bado wanakabiliwa na tatizo hili.
Wadau wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) wakishirikiana na FAWE Tanzania wameendesha mafunzo kwa Klabu za wanafunzi wa Shule za Sekondari wilayani Sengerema, shuhudia walichojifunza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.