TIMU ya Kagera Sugar imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kubaki
Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kulazimisha sare ya 0-0 na wenyeji Pamba SC
jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
Mchezo huo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kubaki na kupanda Ligi Kuu, ulikuwa mkali na wa kusisimua na Pamba SC watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kutumia nafasi walizotengeza.
Kagera Sugar; Ramadhani Chalamanda, Mwaita Gereza, David Luhende, Juma Nyosso, JUma Shemvuni, Peter Mwalyanzi, Suleiman Mangoma, Ally Ramadhani, Ramadhani Kapera, Paul Ngalyoma/Jerson Tegete dk68 na Venende Ludovic/Japhet Makalai dk53.
John Mongella ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa mchezo huo kati ya Pamba Sc iliyokaribisha Kagera Sugar dimba la Nyamagana jijini hapa akisalimiana na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa akiba wa timu ya Kagera Sugar.
Hadi mwisho timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 0-0.
Sasa Kagera Sugar wanarejea nyumbani Bukoba kujipanga kwa mchezo wa marudiano Jumamosi ya tarehe 8 mwezi huu Juni 2019 katika dimba la Kaitaba, wakihitaji ushindi ili kusalia Ligi Kuu.
Kagera Sugar wameangukia katika Play-Off baada ya kumaliza nafasi ya 18 kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wakati Pamba SC ilimaliza nafasi ya pili kwenye Kundi B.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.