Waamini wa
dhehebu wa kanisa katoliki wametakiwa kuenzi na kuhifadhi maeneo ya kistoria ya
kanisa hilo ili historia ya kanisa izidi kuwepo kwa vizazi vijavyo.
Katika
safari ya hija ya kumbukumbu ya wamisionarai waliofika Afrika Mashariki
wakianzia Tanzania na baadae nchini Uganda mahujaji hao wamesema ipo haja ya
historia ya kanisa kuenziwa kwa kuboresha sehemu za historia.
Baada ya
wamisionari kutoka Bagamoyo na Zanzibar walifikia hapa KAGEYE mkoani Mwanza ili kueneza injili kwa kanda ya ziwa na
baadae kuingia nchi jirani Uganda, eneo
hili la kageye linabaki kuwa chimbuko la kanisa hili.
Safari ya
mahujaji hawa kutoka mkoa wa Mwanza kuelekea nchini Uganda ililenga kutembelea
maeneo ya kihistoria ya kanisa katoliki wakianzia Kageye,Bukumbi mkoani Mwanza
ambapo kanisa la kwanza la katoliki lilijengwa, na baadae kuhitimisha na Namgongo nchi
Uganda.Pause
Maeneo ya
kihistoria ya kanisa inadaiwa kukosa muamko wa waamini kutembelea na kujifunza historia
ya kanisa iliyoachwa na wamisionari walifika Afrika kueneza injili ya
kikristo.Pause
Ni miaka 150
sasa ya ukristo tangu dini hii ingie Tanganyika baada ya wamisionari roho mtakatifu kuingia Tanganyika tangu
mwaka 1868 kupitia Bagamoyo na Zanzibar
ili kueneza dini la kikristo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.