Mahakama ya Rufaa imeamua matokeo rasmi ya kura za urais yatatangazwa na wasimamizi wa uchaguzi vituo vya kuhesabu kura kwenye maeneo bunge.
Uchaguzi wa Kenya utafanyika tarehe nane mwezi Agosti mwaka huu ambapo Rais Uhuru Kenyatta atang'ang'ana kuhifadhi wadhifa wake dhidi ya mpinzani wake wa jadi Raila Odinga.
Uamuzi huo wa majaji watano wa Mahakama ya Rufaa umeonekana kama ushindi mkubwa kwa muungano wa upinzani.
Jopo la majaji watanao limesema kwamba mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC hana mamlaka kisheria ya kuhakiki na kutangaza matokeo ya urais.
Msimamo wa tume ya uchaguzi, ni kwamba lazima maafisa wake wahakiki matokeo yote kutoka maeneo bunge katika kituo cha kitaifa cha kuhesabu kura, na kwamba wana uwezo wa kubadilisha matokeo hayo.
Serikali ilikuwa inaunga mkono msimamo huo, japo upinzani ulipinga.
Kwa muda mrefu upinzani umekuwa ukieleza wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa muungano tawala kushirikiana na tume ya uchaguzi kuhujumu matokeo ya uchaguzi.
Tume ya uchaguzi imekana madai hayo.
Uchaguzi wa agosti 8, unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa baina ya rais Uhuru Kenyatta na mpinzani wake mkuu wa muungano wa upinzani NASA, Raila Odinga.
Mahakama hiyo pia ilisema mahakama ya juu ina uwezo wa kisheria wa kutatua mizozo inayotokana na uchaguzi wa urais.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.