ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 22, 2017

WAZIRI MKUU AHIMIZA WATANZANIA KULIPA KODI WAKATI AFUNGUA OFISI ZA TRA, WILAYA YA CHATO.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akikata utepe kama ishara ya kufungua jengo jipya la ofisi ya TRA, Wilaya ya Chato, Mkoani Geita katika ufunguzi uliofanyika leo mjini Chato.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  akipiga makofi baada ya kuwa amekata utepe ambao unaashiria kufunguliwa kwa Jengo la mamlaka ya mapato Wilayani Chato.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akihutubia wananchi wa Chato wakati wa ufunguzi wa jengo la TRA wilayani humo mkoani Geita leo. 

Jengo la mamlaka ya mapato(TRA)Wilayani Chato.

Waziri Mkuu,akiwapongeza na kutoa zawadi kwa kwaya ya Mwagazege  ambao walikuwa wakiimba nyimbo ya kuipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi(CCM)

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakipongeza kikundi cha Kwaya kwa wimbo mzuri.
Mkuu wa Wilaya ya Chato,Shaaban Ntarambe akitambulisha wageni ambao walikuwepo kwenye viwanja hivyo.

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Chato.

Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu waziri wa Nishati na Madini,Dk Medadi Kalemani akizungumza na wananchi.

Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa ofisi ya TRA katika uzinduzi wa ofisi hiyo uliofanyika leo katika wilaya ya Chato, mkoa wa Geita






Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, amesema kuwa kila mwananchi wa Tanzania anawajibika kulipa kodi kwaajili ya ujenzi wa Taifa na kwamba uchumi  utajengwa na watanzania kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa kwani kufanya hivyo itawaza kusaidia upatikanaji mkubwa wa kodi.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa zinduzi wa Jengo la mamlaka ya mapato nchini(TRA)Wilayani Chato Mkoani Geita, ambalo ujenzi wake umeghalimu kiasi cha Sh ,Bilioni 1.4.

Waziri Mkuu amesisitiza  kuwa  Kila mwananchi ambaye anastahili kulipa kodi la lazima alipe bila ya kushurutishwa kwani ni jambo la kawaidia na kwamba nchi ambazo zimeendelea ni kutokana na wananchi wake kujenga destuli ya ulipaji wa kodi

Pia ameendelea kueleza kuwa Kutokana na maelekezo ya Ilani,Katika Mwaka 2016/17 Kuanzia Mwezi Julai,2016 hadi kufikia mwezi Aprili ,2017 Serikali imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilion 20.7 Sawa na Asilimia 70.1 na kwa lengo la mwaka walijiwekea malengo ya kukusanya Sh,Trilion 29.5,Kati ya makusanyo hayo mapato ya ndani ya kodi yalikuwa ni Sh,Trilioni 11.6 Sawa na Asilimia 77.1 ya lengo la kukusanya Sh,Trilion 15.1

Aidha Waziri Mkuu ametoa Wito kwa Kila mwananchi kuakikisha anadai na kupewa Risiti ya manunuzi ya bidhaa alizonunua na kwamba TRA ihakikishe kila mfanyabishara anakuwa na mashine za kielektroniki.


Kamishina wa mamlaka ya mapato TRA Charles Kichere amesema kuwa  Pamoja na kuboresha miundo mbinu ya majengo Mamlaka imeanzisha mifumo ya ukusanyaji mapato kwa njia za kielekitroniki ambazo zitaunganishwa na ofisi hiyo  ili kutoa huduma kwa urahisi kama ilivyo kwenye ofisi zingine kote nchini. 

"Baadhi ya huduma zitakazotolewa hapa ni kama; Utoaji wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN),  utoaji wa leseni za udereva, huduma za usajili wa magari, ukusanyaji wa kodi za majengo, na kodi zinginezo ambazo zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa mujibu wa Sheria"Alisema Kichere.

"Haya yote yanafanyika kwa lengo la kuhakikisha kodi na tozo mbalimbali zilizopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinakusanywa kikamilifu ili kufikia lengo la makusanyo yanayokusudiwa katika mwaka ujao wa Fedha na kuendelea"Aliseongeza Kichere. 

Jengo hilo ambalo  limefunguliwa  leo lilianza kujengwa mnamo tarehe 13 Julai, 2016 na kumalizika tarehe 12 Juni, 2017 ambapo kazi ya ujenzi ilihusisha ujenzi wa jengo la ghorofa moja kama  ambalo lina nafasi ya kutosha kutoa huduma zote za kodi pamoja na huduma za kibenki ili kuwapunguzia adha walipakodi  kwa kupata huduma zote mahala pamoja.


Kampuni ambayo imejenga jengo hilo ni Wakala wa Majengo Tanzania  (TBA)na mjenzi ni kampuni ya Mayanga Constructions ambapo katika ujenzi huu zimetumika kiasi cha Takriban Shilingi Bilioni 1.4.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.