KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva amefunguka kuwa, kitendo cha
Haruna Niyonzima kuondoka kikosini hapo, kimemuachia maswali mengi
yasiyokuwa na majibu, hivyo ataendelea kummisi kila kukicha.
Niyonzima ambaye msimu ujao ataitumikia Simba, ameondoka Yanga baada ya
kumaliza mkataba huku akishindwa kuongeza kutokana na kushindwana
kimaslahi na viongozi wake hao wa zamani.
Akizungumza na Championi Ijumaa,Msuva alisema, kati ya wachezaji wote wa
kigeni aliowahi kucheza nao ndani ya Yanga, Niyonzima ndiye aliyetokea
kuendana naye kwa kila kitu.
“Kwa kweli Haruna nilimzoea kupitiliza, alikuwa kama mtani wangu, hivyo
basi kwa hali hiyo iliyotokea, kwa upande wangu nimeumia sana lakini
sina jinsi.
“Kuondoka kwake haimaanishi kwamba nitashuka kiuwezo, bali nitaendelea
kupambana na nitashirikiana na wengine kama nilivyokuwa nashirikiana
naye.“Nitamisi vitu vingi kutoka kwake, najua hata yeye huko alipo
nadhani anafahamu ameniacha kwenye hali gani, nasema hivyo kwa sababu
kati ya wachezaji wa nje niliowahi kucheza nao, yeye pekee ndiye
nimevutiwa naye,” alisema Msuva.
Ibrahim Mussa
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.