ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 22, 2017

NAIBU KATIBU MKUU CCM AONGOZA MAZISHI YA ALLY YANGA MKOANI SHINYANGA.



Ibada ya mazishi kwa marehemu iliongozwa na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya.

Na Albert G. Sengo

Shinyanga.
HATIMAYE mwili wa aliyekuwa shabiki  kindakindaki wa Dar es salaam Yanga Africans  Ally Said almaarufu Ally Yanga umezikwa hii leo  mkoani Shinyanga kwenye makaburi ya Kiislamu ya Nguzo Nane mkoani hapa.

Mamia ya mashabiki wa soka wa ndani na nje ya nchi wamehudhuria ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwao na marehemu maeneo ya mitaa ya   Stendi kuu ya zamani ambako majonzi na vilio vilisikika hii ikimaanisha Ally Yanga alikuwa kipenzi cha watu.

Naibu Katibu Bara wa chama cha Mapinduzi Fredick Mpogoro akitoa salamu za rambirambi za Serikali.
Ibada ya mazishi kwa marehemu iliongozwa na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya na kwa upande wa serikali iliwakilishwa na Naibu Katibu Bara wa chama cha Mapinduzi Fredick Mpogoro.

Abdallah Rashidi katibu wa tawi la Yanga Mkoa wa Shinyanga amesema kuwa marehemu alikuwa kiunganishi mkubwa kwa mashabiki wa ndani ya mkoa na nje ya mkoa  na alikuwa mhamasishaji mzuri kwenye masuala ya michezo hata ngazi za kitaifa.

Enzi za uhai wake shabiki  kindakindaki wa Dar es salaam Yanga Africans  Ally Said almaarufu Ally Yanga (mwenye suti)
Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi (katikati) akiteta na makada wa CCM kwenye  Ibada ya mazishi kwa marehemu Ally Yanga yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu mjini Shinyanga.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack amesema kuwa serikali imepoteza kijana wa kipekee aliyeunganisha vijana katika uzalendo na kuiasa jamii na vijana waliobaki waige mfano wake.

Naye Naibu Katibu mkuu CCM Fredrick Mporogo akitoa salamu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Chama kinatambua uwezo wa marehemu katika uhamasishaji kwani kupitia sanaa yake aliweza kuwaunganisha watanzania kuzungumza lugha moja hasa kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 hivyo kwa kuliona hilo serikali imetoa ubani kiasi kidogo cha shilingi million 5 ili kuwafariji wafiwa ndugu jamaa na marafiki.
Waombolezaji.
Waombolezaji.
Sehemu ya akinamama waombolezaji.
Sehemu ya akinamama waombolezaji.
Akinamama wakimtuliza dada wa marehemu wakati wa maombolezo.
Huzuni na simanzi vimetawala nyumbani hapa kumpoteza kipenzi cha watu Ally Yanga.
 Awali akisoma wasifu wa marehemu, msemaji wa familia Ali Mwetela amesema marehemu alizaliwa mnamo mwaka 1984 mkoani shinyanga na kupata elimu yake ya msingi kasomea shule ya msingi Mapinduzi hakufanikiwa kuwa na familia.
Mwakilishi wa TFF mkoa wa Shinyanga.


Viongozi, jeshi la polisi, magereza, wapenzi na mashabiki wa soka wamejitokeza hapa kushiriki ibada hatimaye mazishi ya marehemu Ally Yanga.

Mwili wa marehemu ulitolewa ndani ulikohifadhiwa.
Akinamama wakimtuliza dada wa marehemu wakati wa maombolezo.
Mama wa marehemu shabiki  ya Yanga Africans  Ally Said almaarufu Ally Yanga (mwenye kanga ya blue katikati)
Safari ya mwisho ya aliyekuwa shabiki  kindakindaki wa Dar es salaam Yanga Africans  marehemu Ally Said almaarufu Ally Yanga ambaye amezikwa leo kwenye makaburi ya Nguzo nane mkoani Shinyanga.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.