ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 21, 2012

WENJE AJIBU MAPIGO MWANZA, AZUNGUMZIA PIA KUZOMEWA WAZIRI MKUU, ATOA SHAVU KWA LOWASA


"Hata Dokta Slaa akileta noma leo, hata Mbowe, hata Zito, hata Wenje, CHADEMA Itasonga !!! Kwani  CHADEMA ndiyo tumaini la Watanzania iliyobeba Wakristu na Waislamu ambao wana matumaini ya kufika wanapotaka kufika"... 
"Hiki chama ni kikubwa kuliko mimi Wenje ndiyo maana naibu Meya amewaambia kuwa mimi nani alikuwa ananijuwa? Chadema imeanza kabla yangu mimi nikafuatia...." Ni  kauli az Mbunge wa Nyamagana Mhe. Ezekiel Wenje aliyoitoa leo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la wazi kata ya IGOMA wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.


Akizungumzia kuhusu fedha za jimbo (CDCF) Mh. Wenje amesema kuwa kila kata kila diwani awe wa CCM awe wa Chama gani alipewa shilingi milioni tatu  kwa ajili ya maendeleo ya kata yake hivyo siku yaja ambapo kila diwani kwa mipango aliyowasilisha atakwenda kukaguliwa na migao hiyo ya milioni tatu, tatu ni suala la kitaifa.




WENJE Amsifu Lowasa kuwa na ndoto ya kukuza elimu nchini amponda Pinda na mpango wake kuhakikisha kila mtanzania anamiliki mizinga ya nyuki. (SIKILIZA)
Pigo la chini alilokuwa 'katupia pale kati' mhe. mbunge Wenje .....   


WENJE Ajibu shutuma za kununulia watu viroba wamzomee mhe Pinda mkutano wa Sahara Mwanza. (SIKILIZA)
WENJE  Ajibu shutuma za Pinda kuwa CHADEMA imeshindwa kuongoza Halmashauri ya jiji la Mwanza ndiyo maana wanafukuzana. (SIKILIZA)
Wananchi wakimsikiliza Mhe. Ezekiel Wenje katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo ijumaa eneo la Igoma jijini Mwanza.


Wadau kila mtu na umakini wake kusanyikoni...


Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje na watu wake...


Kilichonishangaza tofauti na zama zilizopita nembo, mavazi au alama za vyama vingine zilikuwa zikipigwa marufuku au kuchanwachanwa au hata kuteketezwa maeneo ya makusanyiko kama haya lakini safari hii utulivu amani vimeenea watu wakisikiliza sera. PIG UP!!!!

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.